Wachezaji wa Yanga pamoja na Azam wakiingia
Uwanjani. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
Benchi la
Ufundi la timu ya Azam
Benchi la ufundi la timu ya Yanga
Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu
akiipangua ngome ya Azam kabla ya kuachia kiki kali na kuipatia timu yake bao la
kwanza.
Mshambuliaji wa
Yanga, Simon Msuva (kushoto) akichuana na beki wa Azam, FC, Said Morad katika
mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar
es Salaam. Yanga ilishinda 2-0.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia
Mshambuliaji
wa Yanga Hamisi Kiiza akiwaongoza wachezaji waenzake kushangilia bao la kwanza
la lililofungwa na Didier Kavumbagu (kushoto) wakati wa mchezo wa Ligu Kuu ya
Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga ilishinda 2-0.
Golikipa wa Azam,
Ally Mwadini akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake wakati wa
mchezo wao dhidi ya Yanga.
Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Azam
Raha ya ushindi,
hureeeeeeeeeeee
Balozi
wa Fifa, Abeid Pele (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa TFF pamoja
na Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto wakati alipohudhuria mchezo wa Ligi Kuu ya
Soka Tanzania Bara kati ya Yanga na Azam FC kwenye uliuofanyika leo Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam. Pele yupo nchini kwa ajili ya programu za
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
MOROGORO,
Tanzania
Kutoka mjini Morogoro Simba
ya jijini Dar es Salaam leo imejikuta ikiangukia pua baada ya kuchapwa bao 2-0
na Mtibwa Sugar, mchezo litawaliwa na rabsha za mara kwa mara kutoka kwa
mashabiki wa Simba waliokuwa na hasira wakidai mwamuzi Judith Gamba, alikuwa
hawatendei haki.
Mtibwa ilijipatia bao dakika
ya 34, kwa bao lililofungwa na Mohamed Mkopi baada ya Kipa Juma Kaseja kutema
shuti kali la Vicent Barnabas.
Dakika ya 87, mshambuliaji
mahiri Hussein Javu, aliipatia Mtibwa bao la pili, baada ya Kaseja kufanya
mbwembwe langoni mwake.
Baada ya mchezo kumalizika,
Kaseja aliangua kilio uwanjani huku mashabiki wakimzonga.
Wachezaji wa Simba waligoma
kupanda basi lao, ambako baadhi ya viongozi wao walifanya kazi ya ziada
kuwabembeleza, ambako walikubali kwa shingo upande, lakini baada ya muda Mrisho
Ngasa alishuka akiwa kabadilisha nguo kuondoka kivyake huku akisindikizwa na
mashabiki lukuki.
Yanga iliwakilishwa na
Ally Mustafa Barthez, Mbuyi Twite, Oscar Joshua, Naroub Cannavaro, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Haruna Niyonzima.
Azam: Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Ibrahim Shikanda, Aggrey Morris, Said Morad, Kipre Balou, Salum Abubakar, Jabir Aziz, John Boko, Kipre Tchetche, Hamis Mcha ‘Viali’
Post a Comment