Mwanamke mmoja nchini Marekani amepandishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwaua watoto wawili kwa kuwachoma visu, katika kile kinachoaminika ni kuonesha hasira zake kwa mumewe.
Mwanamke huyo Elzbieta Plackowska mwenye umri wa miaka 40 na mhamiaji kutoka Poland, anatuhumiwa kumuua mtoto wake mwenyewe wa kiume Justin mwenye miaka 7, na mtoto wa kike aliyekuwa akimlea mwenye umri wa miaka mitano.
Mamlaka za jimbo la Illinouis zinasema kwamba Justin alipigwa visu mara 100.
Mkuu wa polisi wa eneo hilo amesema kwamba hilo ni tukio baya kabisa kulishuhudia tangu aanze kazi ya upolisi miongo mitatu iliyopita.
Mwendesha mashitaka amesema kwamba Plackowska alifanya mauaji hayo akiwa na hasira dhidi ya mume wake, dereva wa gari kubwa, na ambaye mara nyingi huwa hayupo nyumbani.
Post a Comment