Farid Mussa Shah wa Serengeto kulia akichuana na beki wa Kongo Brazzaville Tmouele Ngampio katika mechi hiyo |
Na Bin Zubeiry
MECHI ya
mchujo ya Kombe la Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya
Tanzania, Serengeti Boys na Kongo Brazzaville iliyochezwa juzi Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam imeingiza Sh. 23,021,000.
Ofisa Habari
wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo ameiambia leo kwamba,
mapato hayo yametokana na washabiki 18,022 waliokata tiketi kushuhudia pambano
hilo kwa viingilio vya sh. 10,000, sh. 5,000, sh. 2,000 na sh. 1,000. Washabiki
15,850 walikata tiketi za sh. 1,000.
Amesema
asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 3,511,677.97 ilikwenda kwenye Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh.
5,956,635), usafi na ulinzi (sh. 2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch
preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000), umeme
(sh. 300,000) na ulinzi wa mechi (sh. 3,500,000).
Kwa upande
wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 1,000,537, asilimia 10 ya uwanja
sh. 500,269, asilimia 5 ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) sh. 250,134, asilimia
45 ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,251,209, asilimia 20 ya
TFF (sh. 1,000,537) na Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) sh.
50,027.
Post a Comment