Vijana walioshiriki katika uzinduzi wa kinywaji kisichokuwa na kilevi cha Alvaro kinachotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries,wakigonganisha chupa zao kuashiria ishara ya uzinduzi rasmi wa kinywaji hicho hapo jana jijini Da es Salaam.
Mmoja kati ya vijana
akicheza”Break Dance”wakati wa uzinduzi rasmi wa kinywaji kipya kisichokuwa na
kilevi cha Alvaro kinachotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries
LTD.
Baadhi ya vijana
walioshiriki katika uzinduzi wa kinywaji kisichokuwa na kilevi cha Alvaro
kinachotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries wakionesha umahiri
wao wa kucheza katika uzinduzi rasmi wa kinywaji hicho jijini Dar es Salaam hapo
jana.
Warembo walioshiriki
katika uzinduzi rasmi wa kinywaji kipya kisichokuwa na kilevi cha aina ya Alvaro
kinachotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries LTD,Wakionesha
umahiri wao wa kucheza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es
Salaam.
---
NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti imezindua kinywaji kipya
kisicho na kilevi kinachoitwa Alvaro ambacho kimekuwa kikizalishwa muda mrefu
katika nchi nyingine za Afrika Mashariki.
Katika uzinduzi wa aina yake uliofanyika mwishoni mwa
wiki jijin Dar es Salaam, Meneja wa Kinywaji hicho Anita Msangi alisema kinywaji
hicho kitakidhi wateja wanaotumia vinywaji visivyo na kilevi
Uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika katika kumbi za
Mlimani City na Quality Plaza jijini, Dar es Salaam, ulivutia watu kutoka
matabaka mbalimbali ambao walionekana kufuruhishwa na ladha ya kinywaji
hicho.
Akizungumza katika sherehe hizo, Bw. Njowoka aliahidi
watumiaji wa kinywaji hicho na vingine vinavyotengezwa na kampuni ya Serengeti
kuwa kampuni yake imejipanga kuona kuwa wateja wanapata bidhaa bora zenye
viwango vya hali ya juu vinavyostahili na kukidhi matakwa ya wateja
wake.
Pamoja na wageni wengi waliofika kwenye uzinduzi huo,
sherehe za kuzindua kinywaji hicho pia zilipambwa na vikundi mbalimbali vya
vijana ambavyo vilionesha uweso mkubwa katika sanaa ya muziki pamoja na kucheza
dansi.
Kinywaji cha Alvaro kimekua kikizalishwa kwa muda mrefu
katika nchi za Uganda na Kenya kupitia kampuni mama ya kiwanda cha kutengzeneza
bia cha Serengeti iitwayo East African Breweries Limited.
Post a Comment