TANESCO yaibuka mshindi
katika mzunguko wa kwanza
Shirika la Ugavi wa Umeme nchini Tanzania
(TANESCO) limeibuka mshindi wa jumla wa kero kwa wateja wa
huduma mbalimbali na bidhaa hapa nchini kupitia mchakato unaoendelea
kupitia mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook. Nafasi ya pili ilishikiliwa
na Kampuni ya mawasiliano ya Tigo na ya tatu kuchukuliwa na kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom.
Katika
mzunguko wa kwanza jumla ya makampuni 29 yaliingia katika kinyanganyiro na
kufanikiwa kuchukua ushindi katika makundi mbalimbali .
Katika
kundi la huduma za usafiri wa Anga , Shirika la Ndege la Precision ndio
liliongoza kwa kero na huduma zisizo na uhakika huku kundi la huduma za maji
likishikiliwa na Dawasco.
Kwa upande
wa usafiri wa mabasi Kampuni ya Happy Nation iliongoza kwa malalamiko kutoka kwa
wateja huku kundi la ving’amuzi vya Televisheni likiongozwa na Star
Times.
Kwa upande
wa huduma za maegesho ya magari , eneo la Magogoni Ferry limelalamikiwa na
wateja kwa huduma mbovu na kufanikiwa kushika nafasi za juu katika kundi
hilo.
Kwa upande
wa wateja wanaolipia huduma za Televisheni kituo cha TBC pekee ndicho
kimelalamikiwa kwa kutokuwa na huduma za uhakika kwa watazamaji
wake.
Katika
kundi la huduma za mawasiliano ya simu za mkononi , Kampuni ya Tigo ndiyo
iliibuka mshindi ikifuatiwa na Kampuni ya Vodacom.
Zoezi hili
la kukusanya kero linafanywa na Wananchi kupitia akaunti ya Twitter
inayopatikana kupitia @hudumambayatz na facebook group iliyopewa jina la HUDUMA
BONGO ambapo huduma na bidhaa zote zinazolipiwa na wateja mfano Burudani, Elimu,
Hospitali, Hoteli, n.k zinazowakera wateja zitaingia katika kinyanganyiro
hicho.
Washauri
wa kibiashara wa Huduma Bongo wanatoa wito kwa viongozi wa juu wa Mashirika yote
29 yaliyotajwa kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha wateja wao wanapata
huduma bora kulingana na fedha wanazotoa ili kuweza kuleta maendeleo ya
Taifa.
Zoezi hili
linaendelea ambapo katika mzunguko wa kwanza jumla ya kero 119 ziliwasilishwa na
wateja endapo msomaji una kero iliyoshindwa kupatiwa ufumbuzi na watoa huduma
hawa unahitajika kuwa na akaunti inayotambulika ya Twitter au Facebook na
kujiunga na Huduma Bongo kisha ueleze kero yako. Ukweli na Haki kuzingatiwa.
Chanzo:
mjengwa blog



Post a Comment