Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban Ki Moon kwa pamoja na Rais wa Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa,
Bw. Vuk Jeremic, na Rais wa Baraza Kuu la Usalama kwa mwezi wa Novemba, Balozi
wa India, Hardeep Singh Puri wakiwasha mishumaa, ikiwa ni ishara ya kuwaenzi na
kuwakumbuka raia, wanajeshi na polisi 29 ambao wamepoteza maisha katika kipindi
cha kuanzia Novemba 2011 hadi Agosti 2012 wakati wakitekeleza majukumu ya ulinzi
wa Amani katika Misheni 11 za Kulinda Amani za Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa
marehemu hao waliokumbukwa katika hafla hiyo wapo wanajeshi watatu kutoka Jeshi
la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) ambao ni Koplo Yusuf Said Chinguile, Staff
Sajenti, Julius Chacha Marasi na Private Anthony Daniel Paul waliokuwa
wakihudumu katika Jimbo la Darfur.
Baadhi ya wageni
wakiwamo mabalozi na Waambata jeshi wakifuatilia hafla maalum ya kuwaenzi na
kuwakumbuka raia, wanajeshi na polisi 29 waliopoteza maisha katika kipindi cha
kuanzia Novemba 2011 hadi Agosti 2012. Hafla hiyo imefanyika siku ya Jumatano
hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, wengine waliopoteza maisha katika kipindi
hicho wanatoka, Nigeria, Kenya, Rwanda, India, Ethiopia, Niger, Jordan, Syria,
Bangladesh, Sierra leone, Senegal, Brazil, Afghanistan, Togo,
Egypt
Umoja wa Mataifa
jana jumatano umefanya hafla maalum ya kuwaenzi na kuwakumbuka wanajeshi,
polisi na raia ambao wamepoteza maisha wakati wakitekeleza jukumu la kulinda
Amani chini ya Mwamvuli wa Umoja wa Mataifa.
Hafla hiyo
iliyojaa simanzi ya aina yake huku ikisindikizwa na nyimbo za maombelezo
kutoka kwaya maalum, iliwahusu jumla ya wahanga 29 kati yao wakiwamo
watanzania watatu ambao walikuwa Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (
JWTZ).
Wanajeshi hao walikuwa
wakihudumu katika kikosi cha Tanzania kilichoko katika jimbo la Darfur
nchini Sudan, chini ya Jeshi la Pamoja la Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika
maarufu kama UNAMID.
Marehemu Koplo Yusuf
Said Chinguile, Staff Sajent Julius Chacha Marasi na Private Anthony Daniel Paul
walipoteza maisha kati kati ya mwaka huu.
Mbali ya Wanajeshi hao
kutoka Tanzania, nchi nyingine ambazo zimepoteza wapiganaji wao katika
kipindi cha kuanzia Novemba 2011 hadi Agosti 2012, na idadi ya marehemu kwenye
mabano ni Nigeria (5), Togo(1), Sierra
Leone(1),Rwanda(1),Kenya(1),India(2),Jordan(1),Egypty(1),Ethiopia(1),Niger(7),Afghanistan(1),
Senegal(1) , Syria(1), Brazil(1) na Bangladesh(1)
Katika salamu
zake mara baada ya tukio la kuwasha mishuma ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka na
kuwaombea pumziko la milele marehemu hao, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
alikuwa na haya ya kusema.
“ Leo hii tunawakumbuka
wenzetu 29, raia, wanajeshi na polisi ambao wamepoteza maisha katika misheni 11
walikokuwa wakihudumu. Wenzetu hawa wanawakilishi mataifa 16. Kwa kupitia
majina yao na historia yao, tunauona Umoja wa Mataifa, hawa wametoka kila
pembe ya dunia, hawa kuwa na makuu, walijitolea kwa moyo wote kutekeleza jukumu
hili mbali na nchi zao. Baadhi yao wanatoka katika maeneo ambayo yamegubikiwa
na machafuko. Na walikuwa wamedhamiria kuleta amani kwa watu
wengine”.
“
Tunakumbuka heshima ya kufanya kazi na wenzetu hawa, tunajivunia uamuzi na
dhamana waliyoichukua kufanya kazi katika Umoja wa Mataifa. Tunaombeleza pamoja
na familia zao na rafiki zao huku tukienzi uwezo wa kila mmoja wao na mchango
walioutoa kwenye kazi zetu na kwa dunia yetu. Tafadhli ninawaomba muungane nami
kwa dakika mmoja kuwakumbuka ndugu zetu na rafiki zetu”. Akasema Ban Ki Moon,
Katibu Mkuu wa Umoja huo.
Akabainisha kwamba, vifo
hivyo havikupashwa kutokea, lakini ni kielelezo dhahiri cha mazingira magumu na
ya hatari wanayokabiliana nayo wale wote wanaojitolea kuhudumu katika Operesheni
za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.
“Matumaini yangu ni
kutokokea kwa matukio kama haya ambayo si ya lazima, kwamba watu wetu wote
waweza kutekeleza majukumu yao bila ya kuhatarisha maisha yao. Lakini,
tunatambua wazi kwamba Operesheni za kulinda Amani za Umoja wa Mataifga na watu
wote wanaohudumu katika operesheni hizo, wamekuwa wakikabiriwa na mazingira
hatarishi kwa usalama wao” akasema Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa.
Na Kuongeza “ Na
wapumzike kwa amani, wakati tukiendeleza yale waliyokuwa
wakiyafanya”.
Baada ya salamu
za Katibu Mkuu pamoja na zile ziliyotolewa na Rais wa Baraza la 67 la Umoja
wa Mataifa Bw, Vuk Jeremic , Rais wa Baraza Kuu la Usalama kwa mwezi huu wa
Novemba, Balozi wa India, Hardeep Sing Puri ns Bi Paulina Analea Mwakilishi wa
wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, kulifuatia tukio la kusomwa kwa jina moja baada
ya jingine la marehemu hao 29.
Post a Comment