KAMATI
ya kuisaidia timu ya kuisaidia timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17
‘Serengeti Boys’ imeimwagia timu hiyo mil.sita kama motisha kutokana na
kuwafunga vija wenzao wa Congo Brazaville jumapili
iliyopita
Timu hizo zilikutna kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es
Salaam katika mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa vijana wenye umri huo
ambapo Serengeti ilishinda bao 1-0.
Mmakamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kassim Dewji
(pichani)alisema kwamba wameamua kutoa kiasi hicho cha fedha ili kuwapa hamasa
wachezaji wa timu hiyo kujituma zaidi katika mchezo wao wa marudiano ili waweze
kushinda na hatimaye kusonga mbele.
“Tunawapongeza wachezaji wetu kwa kujituma katika mchezo na
vijana wenzao wa Congo Brazaville, hivyo hatuna budi kuwapa fedha hizi kama
motisha ya kuwaweezesha kujiandaa vema na mchezo wao wa marudio,”alisema.
Post a Comment