Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Mh. Halima Mdee akihoji serikali kwa nini ilikuwa ikiwatoza wazazi Sh.70,000 na zaidi ili watoto wao wajiandikishe katika shule za serikali.
Baadhi ya wabunge wanaohudhuria kikao cha bunge mjini Dodoma leo.
Serikali imeendelea kusisistiza kuwa watoto wenye umri wa kwenda shule ya msingi watajiandikisha bila malipo katika shule za serikali hapa nchini Tanzania.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (Elimu) Mh. Majaliwa Majaliwa amesema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kawe (CHADEMA)Mh. Halima Mdee aliyetaka kujua kwa nini wazazi wanalazimika kulipia kiasi cha Sh. 70,000 na zaidi ili kuwaandikisha watoto wa darasa la kwanza.
Mbunge Halima pia alitaka kujua ni kiwango gani cha chini na cha juu ambacho serikali ilipanga kwa ajili ya fedha za kuchangia maendeleo ya shule za msingi na za sekondari hapa nchini
Naibu Waziri Mh. Majaliwa amewaambia wabunge kuwa kwa sasa serikali ilikuwa haijapanga kiwango cha chini na cha juu ikiwa ni michango kwa shule za serikali hapa Tanzania.
Hata hivyo Mh. Majaliwa amesema kuwa serikali ilipanga ada ya Sh 20,000 kwa shule za kutwa za serikali hapa Tanzania.
Post a Comment