MSANII Hussein Ramadhani Mkiete anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwao, Tanga.
Kwa mujibu wa Diwani Makame Seif ambaye ni rafiki wa karibu marehemu, aliyefarfiki kwa ajali Saa 2:00 usiku jana eneo la Maguzoni Tanga, Polisi wametambua ni Sharo Millionea kwa vitambulisho vyake na picha moja ya passport aliokuwa nayo mfukoni ambavyo kwa sasa viko na polisi.
Diwani huyu amemfahamisha mwandishi kuwa Sharo Millionea ameumia vibaya sana kichwani, kifuani na kwenye mikono. Pia Mjomba wa marehemu amethibitisha kuwa Sharo Millionea atazikwa Tanga na asubuhi ya leo ratiba ya msiba itatolewa. Ndugu na marafiki wa Sharo wameanza kwenda hospitalini baada tu ya taarifa hizi kuwafikia. Familia ya Sharo imeshafika Hospitali ya Teule ya Tanga.
Wadau mbali mbali wa tasinia ya burudani wameonyesha kusikitika na kuhuzunishwa na kifo cha msanii mahiri wa vichekesho nchini Sharomilionea
KITALE
akihojiwa na TBC akiongea akiwa na majonzi ya hali juu alisemaa alishindwa
kuamini kama kweli sharo kafariki mpaka alipompigia simu mzee majuto
nakumthibitishia kweli tukio ndo hilo aliishiwa nguvu baada ya kuthibitishiwa
habari nakusema amempoteza mtu mhimu sana kwake binafsi na hajui itakuwaje.na
alishindwa kujizuia kulia
Steve
nyerere nae alipohojiwa na TBC nae alionyesha kusikitishwa na kifo cha msanii
huyo nakusema ameacha pengo kubwa katika tasnia hiyo ya comedy
Jackson
Mbando wa airtel akiongea na clouds fm katika kipindi cha power breakfast
alisema kuwa nipigo kubwa katika tasnia zima ya burudani na airtel
wameskitishwa na kuumia sana kutokana na kifo cha msanii huyo ukizingatia
alikuwa mdau wao mkubwa amnetegeneza matamngazo na airtel
R.I.P
SHARO MILLIONEA
Post a Comment