Makamu Mwenyekitin wa CCM, Dk. Shein |
Maelfu ya
Wana-CCM na wananchi kwa jumla, wanatarajiwa kufurika leo kwenye Viwanja vya
Demokrasia (zamani, Kibandamaiti), wakati wa sherehe kubwa ya kupongeza safu
mpya ya uongiozi wa CCM kitaifa uliochaguliwa wakati wa mkutano mkuu wa CCM
ulimalizika juzi juzi mjini Dodoma.
Kulingana
naratiba iliyopatikana, sherehe hizo zitarindima kuanzia saa tisa alasiri, na
safu karibu yote ya uongozi huo itakuwepo, isipokuwa mwenyekiti wa CCM, Taifa,
Rais Jakaya Kikwete na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip
Mangula.
Imethibitishwa
kwamba, kwenye sherehe hizo watakuwepo Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Rais wa
Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, Naibu Katibu Mkuu (Bara) Mwigulu Nchemba,
Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Vuai Ali Vuai, Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye,
Katibu wa Uchumi na Fedha Zakia Meghji, Katibu wa NEC Oganaizesheni Mohammed
Seif Khatib na Katibu wa NEC, Siasa na mambo ya Nje, Dk. Asha-Rose Migiro
Post a Comment