Na Mahmoud
Zubeiry
BAO pekee la
Mussa Said Kimbu dakika ya 73, leo limeizamisha Simba SC kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara.
Kimbu
alifunga bao hilo akiunganisha krosi ya Mganda, Mohamed Jingo tena akipitisha
mpira katikati ya msitu wa mabeki wa Simba na kipa wao, Wilbert
Mweta.
Simba
hawakucheza vizuri kama timu leo, ila kwa mchezaji mmoja mmoja, karibu kila
mchezaji alicheza vizuri na Emanuel Okwi ndiye aliyekuwa akiisumbua zaidi ngome
ya Toto.
Katika
michezo mingine ya ligi hiyo, Azam imefungwa 2-1 na Mgambo JKT Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga.
Kwa matokeo
hayo, Yanga inazidi kujinafasi kileleni kwa pointi zake 26, baada ya kucheza
mechi 12 na kesho itahitimisha mechi zake za mzunguko wa kwanza kwa kucheza
Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Simba
inaendelea kubaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 23 na Azam yenye pointi 24 ni
ya pili.
Simba SC:
Wilbet Mweta, Nassor Masoud ‘Chollo’, Paul Ngalema, Komanbil Keita, Shomary
Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto/Edward Christopher, Mrisho
Ngassa/Haruna Chanongo, Felix Sunzu na Emanuel Okwi.
Toto; Erick
Ngwengwe, Ally Ahmad, Eric Murilo/Robert Magadula, Evarist Maganga, Peter
Mutabuzi, Hamisi Msafiri, Emanuel Swita/James Magafu, Kheri Mohamed/Mohamed
Hussein, Mohamed Jingo, Suleiman Kibuta na Mussa Said.
Post a Comment