Ofisa
Habari wa Simba, Ezekiel
Kamwaga
UONGOZI wa Simba SC unapenda kuzungumza yafuatayo kuhusiana na
matukio ya karibuni kuhusiana na klabu ya Simba.
- Uongozi umesononeshwa na
matokeo ya siku za karibuni ya timu ya Simba hususani yale ya kufungwa mabao 2-0
na Mtibwa Sugar ya Morogoro. Kutokana na hali hiyo, Kamati ya Utendaji ya Simba
imeliagiza benchi la ufundi la Simba kutoa ripoti kuhusiana na mwenendo wa timu
katika mechi za karibuni.
Ikumbukwe kwamba Simba
ilianza ligi kwa vishindo na hadi kufikia mechi ya 12, ilikuwa ikiongoza ligi na
ilikuwa timu pekee ambayo haikuwa imepoteza mechi.
Mara baada ya ripoti ya
benchi la ufundi kukamilika, Kamati ya Utendaji ya Simba itakutana na kutoa
maamuzi kuhusiana na yaliyomo kwenye ripoti. Kutokana na hali hiyo, uongozi
unaomba wapenzi na wanachama wake kuwa watulivu katika kipindi hiki ambapo
uongozi na benchi la ufundi linatafuta suluhisho la kudumu kuwezesha timu
kuendelea kushinda.
Hata hivyo, uongozi wa
Simba unasisitiza kwamba hakuna kiongozi yeyote wa Simba –kuanzia wa juu zaidi
hadi wa chini zaidi, ambaye amejiuzulu au kuachia ngazi ndani ya
klabu.
Ifahamike kwamba uongozi
huu ulipewa dhamana na wanachama miaka minne iliyopita ya kuiongoza klabu kisasa
na kuipa maendeleo endelevu kwa kipindi hicho.
Chini ya uongozi huu, Simba
ilikuwa mshindi wa pili misimu miwili iliyopita (ikiwa pointi sawa na mabingwa
ila ikizidiwa kwa pointi, ilikuwa mabingwa msimu uliopita, iliingia hatua ya 16
bora michuano ya CAF, imesajili wachezaji msimu huu kwa fedha zake yenyewe
(miradi mbalimbali) na inaendesha timu tatu za vijana.
Bado kuna kazi za kufanya
na uongozi unatambua hilo . Ndiyo maana uongozi
hauamini kwamba maneno mabaya yanayosambazwa dhidi ya viongozi yanatoka kwa
wanachama wake. Kazi nzuri ya uongozi huu inaonekana na iko
dhahiri.
Uongozi wa Simba unaomba
wapenzi na wanachama wake kuwa wamoja katika kipindi hiki ili kuwezesha ushindi
kupatikana dhidi ya Toto African ya Mwanza Jumamosi
ijayo.
2. Kuhusu mchezaji Juma
Kaseja
Uongozi umesikitishwa na
vitendo ambavyo baadhi ya washabiki walivifanya dhidi ya nahodha wa Simba, Juma
Kaseja. Washabiki hao walimtukana, kumkashifu, kumdhihaki na kumtishia maisha
mchezaji huyo mara baada ya mechi dhidi ya Mtibwa.
Kaseja ni miongoni mwa
wachezaji wanaoheshimika sana ndani na nje ya
nchi. Vitendo vya kumkashifu si vya kiungwana na uanamichezo. Nahodha huyu
ameitumikia Simba kwa moyo mmoja na ni mmoja wa wachezaji wenye
kuheshimikasana miongoni mwa
wachezaji.
Hatua ya kumtukana
inaharibu heshima ya klabu. Ni mchezaji mgani mzuri atataka kujiunga na Simba
iwapo ataona Kaseja anafanyiwa hivyo? Benchi la ufundi la Simba ni makini na
iwapo kutakuwa na tatizo lolote la kiuchezaji, litafanya
mabadiliko.
Kama Kaseja angekuwa
anapendelewa Simba, asingechaguliwa kuwa kipa namba moja wa Taifa Stars na
nahodha pia.
Tunachukua fursa hii
kutangaza kwamba uongozi wa Simba, kuanzia sasa, hautavumilia matusi kwa
wachezaji au viongozi wake. Wote watakaobainika kufanya matendo haya, sheria
itachukua mkondo wake.
Imetolewa
na
NA BIN
ZUBEIRY
Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga |
UONGOZI wa Simba SC unapenda kuzungumza yafuatayo kuhusiana na
matukio ya karibuni kuhusiana na klabu ya Simba.
- Uongozi umesononeshwa na matokeo ya siku za karibuni ya timu ya Simba hususani yale ya kufungwa mabao 2-0 na Mtibwa Sugar ya Morogoro. Kutokana na hali hiyo, Kamati ya Utendaji ya Simba imeliagiza benchi la ufundi la Simba kutoa ripoti kuhusiana na mwenendo wa timu katika mechi za karibuni.

Post a Comment