Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

M-Pesa Kunufaisha Watanzania Zaidi

 



Katika kuendeleza azma yake ya kuwawezesha wananchi kubadili maisha kupitia teknolojia ya simu za mkononi, kampuni ya Vodacom Tanzania sasa inawawezesha wateja wake kutumia huduma ya M-pesa kwa faida zaidi katika kila muamala wa utumaji wa pesa.
Kupitia uwezeshaji huo sasa mteja wa Vodacom anaetuma pesa kwa njia ya M-pesa atapokea muda wa hewani BURE wenye thamani sawa na gharama alizotozwa wakati akituma pesa hizo kwenda sehemu yoyote nchini mara tu amalizapo zoezi la kutuma pesa hizo.
Akizungumzia kampeni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza amesema hiyo ni njia moja ya kuwashukuru wateja zaidi ya Milioni Nne na Nusu wanaoendelea kuiamini huduma ya M-pesa na kuitumia kila siku katika shughuli zao mbalimbali.
"Mteja haitaji kujisajili kunufaika na kampeni hii na wala hatotumia muda kupokea muda wa hewani wa BURE Vodacom itampatia shukrani yake ya muda wa hewani kwa kutumia M-pesa mara tu atakapomaliza kutuma fedha hizo kwenda kwa mteja wa Vodacom sehemu yoyote hapa nchini."Aliongeza Meza Chini ya kampeni hii, wateja wa Vodacom wanapata zaidi cha kujivunia katika huduma yao ya M-pesa huku wakiwa na wigo mpana zaidi wa kufurahia mawasiliano kupitia mtandao wa Vodacom kwa kuwa na salio la ziada la kufanya hivyo.
"Ni fursa nyengine kwa wateja wetu kufurahia kila watumapo pesa kwa M-pesa huku wakipata cha ziada kufurahia kuwa wateja wa Vodacom kwa kuongea zaidi miongoni mwao."Aliongeza Meza Tangu ilipoanzishwa Aprili, 2008 huduma ya M-pesa imebakia kuwa huduma bora, salama, ya uhakika na yenye kuaminika kwa watanzania ikiwa na mtandao mpana zaidi wa mawakala wanaofikia 40,000 mijini na vijini na hivyo kuifanya huduma hiyo kuwa mkombozi wa jamii kwa huduma za kibenki hapa nchini.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top