Onyesho
kubwa la mitindo la Afrika Mashariki na kati linarajiwa kufanyika siku tatu
mfululizo katika Hoteli ya Golden Tulip kuanzia tarehe 6, 7 na 8 Desemba, 2012
ikiwa ni mara ya tano tangu kuanzishwa kwake.
Swahili
Fashion Week 2012 kwa ujumla itakutanisha pamoja wadau 50 katika tasnia ya
Mitindo kutoka nchi zinazozungumza Kiswahili na nyengine kuweza kuonyesha
ubunifu wao na kutoa mustakabali wa mwenendo wa tasnia ya mitindo katika ukanda
huu.
“Mwaka
tumekuwa kwa kiasi kikubwa, wabunifu 23 kutoka Tanzania wataweza kuonyesha
ubunifu wao na wengine waliobaki ni kutoka nje ya Tanzania, ambao wote
wataonyesha ubunifu wao katika jukwaa moja ukiachilia wabunifu 16 walionyesha
ubunifu wao katika maonyesha ya Swahili Fashion Week yaliyofanyika Nairobi,
Kenya, Oktoba 6, 2012” Alisema Meneja wa Swahili Fashion Week, Washington
Benbella
Katika
kuongeza maonyesho ya mitindo, mwaka huu Swahili Fashion Week shopping Festival
ambayo ilianza 2010 itakuwepo tena kwa mara nyengine ambapo itashirikisha zaidi
ya waonyeshaji 30 katika sehemu moja ikiwa ni kwa ajili ya kuonyesha na kuuza
bidhaa za ubunifu hivyo kuifanya kuwa msimu mkubwa manunuzi ya kazi za ubunifu
wa mitindo hapa Tanzania.
Kama
ilivyo ada, Swahili Fashion Week inatoa nafasi kwa kuendeleza vipaji, ambapo
tarehe 24 Novemba, 2012 kutakuwa na mchujo wa wazi kwa wanamitindo wapya na
wanaochipukia kwa jinsia zote, na mnamo tarehe 7 Desemba, 2012 kutakuwa na
warsha kwa ajili ya wabunifu wote Tanzania chini wadhamini wakuu wa warsha hiyo
USAID Compete ambayo itafanyika katika Hotel ya Golden Tulip” Aliongeza
Benbella
Mashindano
tofauti yamepangwa kufanyika wakati wa Swahili Fashion Week, ikiwemo Shindano la
kumtafuta Mbunifu Bora anaechipukia na Mbunifu Bora wa kubuni Fulana. Sio tu
inatoa changamoto na ari ya ushindani katika tasnia ya ubunifu nchini Tanzania,
bali pia inaweka msingi imara kwa wabunifu wa baadae.
“Sherehe
maalum za kufungua Swahili Fashion Week zinarajiwa kufanyika siku ya Jumapili
tarehe 25 Novemba, 2012, Thai Village kuanzia saa 9 usiku. Sherehe hizo pia
zitafuatiwa na kutangazwa kwa majina ya waliochaguliwa kushindania tuzo
mbalimbali zilizowekwa katika vipengele 16, tuzo hizi ni za kwanza na ndio pekee
katika ukanda huu. Tiketi za sherehe za uzinduzi wa Swahili Fashion Week 2012
zinapatikana sehemu zifuatazo, Thai Vilage, Mgahawa wa Epidor uliopo Masaki, na
Tanzania Mitindo House” Alisema Meneja Uhusiano, Hassan
Mrope
“Tukiwa
na mipango yenye ndoto za kutangaza biashara ya mitindo katika ukanda wa Afrika
mashariki na kati, ninapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru washirika wetu
pamoja na wadhamini wetu ambao karibia ya wote wamekuwa wakitusaidia kutokea
maonyesha yaliyopita mpaka sasa. Pia tuwashukuru sana watu wote wanaosaidia
tasnia ya mitindo hapa Tanzania kwa si tu kuhudhuria matamasha na maonyesho kama
haya bali pia kwa kununua bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini kwani hii
inatangaza kinachotengenezwa Africa “Made in Africa”. Alimalizia
Benbella
Swahili
Fashion Week 2012 imedhaminiwa na Vodacom, USAID Compete, Origin Africa, EATV,
East Africa Radio, Golden Tulip Hotel. Amarula, Precision Air, 2M Media, Global
Outdoor Ltd, Vayle Springs Ltd, Eventlites, Ultimate Security, BASATA (Baraza
La Sanaa Tanzania), Perfect Machinery Ltd, Ndibstyles, PKF Tanzania and 361
Degrees.
Post a Comment