Mstahiki
Meya akifungua Tamasha.
Mama
Balozi akiwaonyesha wageni Rasmi Mameya vitu mbalimbali vitakavyouzwa kwa ajili
ya kuchangia mfuko huu.
Mtahiki Meya akiangalia sehemu ya chakula
ya Tanzania.
kutoka Kushoto Mh balozi wa Grenada Ruth
Elizabeth Rouse, Mtahiki Meya Christopher Buckmaster na Mama Balozi Joyce
Kallaghe.
Mama
Kiondo akiwa kikazi zaidi kuitangaza Tanzania Pics .
Mama
Balozi Akipakwa Hina kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa
elimu
Mama
Balozi akimkabidhi Mayorese Mrs. Anne Hobson baada ya kununua kitenge katika
banda la Tanzania .
Mayorese Mrs. Anne Hobson katika banda la
Tanzania.
wateja wakinunua bidhaa kutoka banda la
Tanzania.
Sherehe ikiendeleaPics By Frank
Eyembe.
Ukumbi wa Royal Borough of
Kensington.Pics By Frank Eyembe.
---
Salaam,
Jumuiya ya Commonwealth Countries League
(CCL) inayoshirikisha nchi hamsini na nne (54) duniani kutoka katika jumuiya ya
madola iliandaa tamasha maalum siku ya jumamosi tarehe 3.11.12 kwa ajili ya
kuchangia mfuko wa kumsaidia na kumwezesha msichana kusoma elimu ya
sekondari.
Historia ya Commonwealth Countries League
ilianzishwa rasmi kutoka kwa baadhi ya wanawake mnamo mwaka 1923 nchini
Australia kwa ajili ya kusaidia kutangaza uelewa wa haki sawa kati ya wanawake
na wanaume waliopo nchi mbalimbali zilizo ndani katika jamuiya ya
madola.
Tamasha hili lilifanyika Royal Borough of
Kensington chini ya uongozi kutoka kwa Mh. Balozi wa Grenada Ruth Elizabeth
Rouse ambaye ndio raisi wa jumuiya hiyo akisaidia na makamu wake mama Balozi
Joyce Kallaghe. Wageni Rasmi walikua Wastahiki Mameya wa Worshipful Royal
Borough of Kensington na Chelsea - Councillor Christopher Buckmaster na Mrs.
Anne Hobson Shughuli ya mwaka huu iliandaliwa na wake za mabalozi kutoka katika
jumuiya za Madola hamsini na nne (54) ili kuchangisha pesa kwa njia ya kuuza
vitu mbalimbali vya asili kama chakula, urembo, maua, vinywaji n.k. Fedha zote
zilizopatikana zilipelekwa kusaidia mfuko huu wa Elimu kwa ajili ya kumsomesha
mtoto wa kike.
Aidha Mama Balozi Joyce Kallaghe aliongeza
kwa kusema ''Elimu ni Ufunguo Wa Maisha kumsomesha mwanamke ni kuiwezesha jamii
nzima hivyo vipaumbele vyote vimeelekezwa kwa kwa ajili ya kuwasomesha watoto wa
kike walio maskini au wanaoishi katika mazingira magumu ambao wana uwezo wa
kuendelea kusoma elimu ya sekondari katika nchi za jumuiya ya Madola". Tangu
mwaka 2011/2012 mfuko wa Elimu wa CCL ushawawezesha watoto wa kike 364 kutoka
nchi 25 ikiwapo Tanzania. Pia aliwasihi wadau kuwa wazalendo kwa kuchangia
mfuko huu kwa kuwasiliana kupitia barua pepe ccl.edfund@googlemail.com
Kiasi cha paundi mia moja hamsini (£150) na
Mia nne na hamsini (£450) zinatosha kumsomesha msichana kwa mwaka
mzima
Asanteni
Urban
Pulse Creative
Post a Comment