Na
Mwananchi Online
TETEMEKO limeendelea
kulikumba Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kutokana na mamia ya wafanyakazi
wa shirika hilo kupanguliwa kama hatua ya kuvunja mtandao wa wizi na hujuma
ndani yake.
Habari ambazo Mwananchi lilizipata na kuthibitishwa na uongozi wa juu wa Tanesco zinasema hadi sasa wafanyakazi 190 wa Tanesco wameshakabidhiwa barua za kuhamishwa na nusu ya watumishi hao ni katika Mkoa wa Dar es Salaam pekee.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, wafanyakazi 95 wamepanguliwa kutoka katika mikoa ya Tanesco iliyopo katika Jiji la Dar es Salaam pekee na wamehamishiwa mikoani ambako wanatakiwa wawe wameripoti katika vituo vyao vipya vya kazi ifikapo Novemba 15, mwaka huu.
Kadhalika idadi kama hiyo ya watumishi kutoka mikoani wamehamishiwa Dar es Salaam, hatua ambayo inalenga kuimarisha utendaji katika jiji hilo ambalo licha ya kuwa kitovu cha uchumi wa nchi, huduma za Tanesco zimekuwa zikilalamikiwa kuwa haziridhishi.

SOURCE/SOMA ZAIDI MWANANCHI ONLINE
Post a Comment