Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule, akifungua Mkutano wa Timu ya
Pamoja ya Wataalam kati ya Tanzania na Malawi kuhusu mgogoro wa
mpaka kwenye Ziwa Nyasa. Mkutano huo uliowahusisha wataalam kutoka
Wizara na Idara mbalimbali za Serikali za Tanzania na Malawi unafanyika Jijini
Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena.
Bw. Julius Chisi, Naibu Mpimaji
Ardhi Mkuu kutoka Malawi akizungumza machache wakati wa mkutano
huo.
Bw. Abdallah Mtibora, Afisa kutoka
Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa
akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
kufungua mkutano huo.
Baadhi ya Wajumbe kutoka Tanzania
akiwemo Mhe. Balozi Patrick Tsere (wa pili kutoka kushoto), Balozi wa Tanzania
nchini Malawi na Balozi Irene Kasyanju (kushoto) wakimsikiliza Bw. Chisi (hayupo
pichani) wakati wa akizungumza.
Baadhi ya Wajumbe wengine kutoka
Malawi akiwemo Mhe. Chiyaonga (kulia), Balozi wa Malawi hapa
nchini.
Sehemu nyingine ya Ujumbe wa
Tanzania kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wajumbe kutoka Malawi
wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano
huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule akizungumza na Mhe. Flosie Gomile
Chiyaonga, Balozi wa Malawi hapa nchini kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Timu ya
Pamoja ya Wataalam wa Tanzania na Malawi kuhusu mgogoro wa mpaka kwenye Ziwa
Nyasa.Picha na Habari- Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa
--
Mkutano
kati ya Tanzania na Malawi kujadili suluhu ya mgogoro wa mpaka kwenye Ziwa Nyasa
umeanza katika ngazi ya Wataalamu jijini Dar es Salaam tarehe 15 Novemba,
2012.
Mkutano huo
unaowahusisha wataalam kutoka Wizara na Idara mbalimbali za Serikali za Tanzania
na Malawi unafanyika Jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya
Serena.
Akifungua
Mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bw. John M. Haule alisisitiza umuhimu wa wajumbe kutoka nchi zote mbili kujadili
na kupendekeza njia zitakazosaidia kupata suluhisho la kudumu la mgogoro
huo.
Aidha, Bw.
Haule aliweka bayana kuwa Serikali ya Tanzania ina dhamira ya dhati kufanya kazi
pamoja na Serikali ya Malawi kutafuta suluhu ya mgogoro huo jambo ambalo pia
lilisisitizwa na Bw. Julius Chisi, Kiongozi wa Ujumbe wa
Malawi.
Mkutano huo
ambao utafanyika kwa siku tatu hadi tarehe 17 Novemba, 2012 umeanza na Kikao cha
Wataalamu ambacho kitafuatiwa na kikao cha Maafisa Waandamizi na kuhitimishwa na
kikao cha Mawaziri tarehe 17 Novemba, 2012.
Post a Comment