CHAMA
cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimeamua kulipeleka kwa
Chama chaWamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), suala la kuzuia
televisheni na redio kutangaza moja kwa moja michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara
pamoja na wapiga picha za televisheni kuchukua picha kwa ajili ya kutumia kwenye
habari.
Hatua hiyo ya TASWA ina
lengo la kuomba mwongozo kwa chama hicho ambacho ndio kinachomiliki vyombo vya
habari kuhusiana na suala hili ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa kiasi kikubwa
na wanachama wetu.
Tayari TASWA imefanya
mazungumzo ya awali na MOAT, ambayo imeridhia iandikiwe barua rasmi ili jambo
hilo lijadiliwe kwenye vikao vyake na baada ya hapo TASWA itapewa mwongozo ambao
itautoa kwa waandishi wa habari za michezo.
Kwa kuwa Mwenyekiti wa
TASWA, Juma Pinto pia ni mjumbe wa MOAT, basi suala hilo tunaamini litafanyiwa
kazi haraka iwezekanavyo, hivyo tunawaomba waandishi wa habari za michezo
waendelee kuwa watulivu na wavumilivu kipindi hiki na wafanye majukumu yao kama
kawaida.
Siku zote chama chetu
kimekuwa na uhusiano mzuri na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wadau wengine
wote na TASWA haitaki ifike mahali iwe na mgogoro na chama chochote cha michezo,
lakini pia haitakuwa tayari kuona wanachama wake wakishindwa kutekeleza majukumu
yao.
Kama mnavyojua wiki
iliyopita kulifanyika kikao cha Kamati ya Ligi na baadhi ya klabu zinazoshiriki
ligi hiyo kuhusiana na tukio la kuzuia televisheni na redio kutangaza moja kwa
moja michezo ya Ligi Kuu pamoja na wapiga picha za televisheni kuchukua picha
kwa ajili ya kutumia kwenye habari.
Katika kikao hicho ambacho
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto alihudhuria kulitoka maelezo mbalimbali ambayo
baadhi ya wanahabari hawakubaliani nayo na wamekuwa wakitaka TASWA ichukue hatua
uamuzi mgumu.
Sekreterieti ya TASWA
imeona si vizuri kukurupuka kuchukua uamuzi wowote ule kwa sasa kwani yenyewe
haina chombo cha habari, lakini wanaofanya kazi kwenye vyombo vya habari ndiyo
wanachama wake. Itawasilisha MOAT maazimio ya kikao cha Kamati ya Ligi kuhusiana
na jambo hili, tuna hakika tutalimaliza
Post a Comment