Kulikuwa na vurugu zisizokuwa za kawaida
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mfalme Khaled jijini Riyadh baada ya
kuwasili kwa kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kujiandaa na mechi yao ya
kimataifa ya kirafiki dhidi ya Saudi Arabia kwenye Uwanja wa Mfalme Fahd kesho
Jumatano.
Maafisa wa Uwaja wa Ndege walilalamikia
kitendo cha maelfu ya mashabiki kufika uwanjani na kulazimisha wapewe nafasi ya
kumuona nyota wa Argentina na klabu ya Barcelona ya Hispania, Lionel
Messi.
Licha ya ulinzi mkali wa polisi waliokuwa na
silaha za moto kwenye uwanja wa ndege na pia katika barabara nzima ya kuelekea
uwanjani, bado mamia ya mashabiki wa Messi walifanikiwa kupenya na kufika
uwanjani.
Straika huyo alifika jijini Riyadh kwa ndege
yake binafsi pamoja na familia yake kabla ya kuwasili kwa wachezaji
wengine.
Hata hivyo, askari kibao waliokuwa uwanjani
walitumia 'akili' za ziada kuwapiga chenga mashabiki na kufanikiwa kumuondoa
Messi uwanjani.
Mashabiki wengi na maafisa wa usalama
walilaumu vurugu za kulazimisha kumuona Messi kweny uwanja wa ndege, wakisema
kwamba ishara hiyo si nzuri kwa timu ya taifa ya Saudi.
Waandishi wa habari pia walikuwa na kazi
kubwa ya kuripoti tukio la ujio wa Messi na wenzake kwani walizuiwa kuwapo
kwenye ukumbi ambao wachezaji walikusanyika.
Habari na http://straikamkali.blogspot.com
Post a Comment