Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TASWIRA ZA KABLA NA BAADA YA KUTANGAZWA KWA MATOKEO YA MWENYEKITI NA MAKAMU WA CCM, DODOMA


Rais Jakaya Kikwete kisikiliza matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa yakitangazwa na Mhe. Anna Makinda
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa CCM (bara)) Phili Mangula (katikati) na Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM,Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakifurahia jambo katika Mkutano Mkuu wa CCM uliomalizika Novemba 13, kwenye ukumbiwa Kizota Mjini Dodoma . (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)

Wajumbe wakiserebuka baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangazwa kuwa mshindi wa Uenyekiti wa CCM, Taifa.

 

Kikwete, akipongezwa na baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipongezwa na aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Makamu wenyeviti wawili, Spika wa Bunge Anna Makinda, baada ya kumtangaza kushinda nafasi hiyo ya Uenyekiti, katika uchaguzi uliofanyika hivi punde katika ukumbi wa Kizota, Dodoma, ikiwa ni kuhitimisha shughuli za Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM. Wapili Kulia ni Makamu Mwenyekiti Mpya wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Dk. Moahamed Gharib Bilal
Mwenyekiti mpya kwa mara nyingine wa CCM Taifa, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akipongezwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mara baada ya kutangazwa kuibuka kidedea kwa kura za asilimia 100 katika uchaguzi, uliomalizika hivi punde katika Ukumbi wa Kizota, mjini Dodoma.
Mwenyekiti mpya kwa mara nyingine wa CCM Taifa, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akipongezwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa wa Zanzibar, Aman Karume, mara baada ya kutangazwa kuibuka kidedea kwa kura za asilimia 100 katika uchaguzi, uliomalizika hivi punde katika Ukumbi wa Kizota, mjini Dodoma.
Mwenyekiti mpya wa CCM Taifa kwa mara nyingine, Jakaya Mrisho Kikwete, akifurahia na kucheza kwa furaha baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo na yeye kuibuka kidedea kwa kura za asilimia 100.

 

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa, akipita kumpongeza Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa, Jakaya Kikwete, baada ya kutangazwa matokeo hayo leo katika Ukumbi wa Kizota, mjini Dodoma.

Mwenyekiti mpya kwa mara nyingine wa CCM Taifa, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akipongezwa na mkewe Mama Salma Kikwete, mara baada ya kutangazwa kuibuka kidedea katika uchaguzi, uliomalizika hivi punde katika Ukumbi wa Kizota, mjini Dodoma. Wengine waliotangazwa katika kinyang'anyiro hicho ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Phillip Mangula, Makamu Mwenyekiti, Zanzibar na Dkt. Ali Mohamed Shein.

Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete akiongoza kikao baada ya kushinda tena kiti hicho. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Ali Mohamed Sheni na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Phili Mangula





Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top