Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii
wa Vodafone group, Andrew Dunnet akikagua moja ya mabasi yatakayo tumika kubeba
wagonjwa wa Fistula, mabasi hayo yamenunuliwa katika mpango wa kupambana na
Fistula uliochini ya CCBRT, Wizara ya Afya na Vodafone uliozinduliwa na Rais
Jakaya Kikwete Februali 25.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya walemavu
ya CCBRT, Dr. Wilbroad Peter Slaa akimuonyesha maendeleo ya ujenzi Mkurugenzi wa
kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet wakati alipofanya
ukaguzi wa wodi za hospitali hiyo kabla ya kukabidhiwa kwa Rais Dk, Jakaya
Mrisho Kikwete mapema mwezi huu.
Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma wa
Vodafone Group, Andrew Dunnet akisikiliza maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi
Kutoka kwa Mtaalamu wa Masuala ya Ujenzi wa Hospitali Tom Bourel wakati
alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa wodi za wagonjwa wa fistula kabla ya kukabidhiwa
kwa Dk. Jakaya Kikwete mapema Mwezi huu, Pamoja nao ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Hospitali ya CCBRT, Dk. Peter Slaa.
Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Margaret Mhando, akipokea zawadi kutoka kwa moja ya
wagonjwa wa Fistula wanaotibiwa katika hospitali ya CCBRT wakati alipofanya
ukaguzi wa wodi mpya za wagonjwa wa fistula kabla ya kukabidhiwa kwa Rais. Dk.
Jakaya Mrisho Kikwete. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa Idara ya huduma za jamii wa
Vodafone group, Andrew Dunnet.
Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma wa
Vodafone Group, Andrew Dunnet akisikiliza maelezo kutoka kwa moja ya wauguzi wa
wodi za wagonjwa wa Fistula wa hospitali ya CCBRT, alipofanya ukaguzi wa wodi
hizo kabla ya kukabidhiwa kwa Rais, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete mapema Mwezi huu.
Pamoja nao ni Mwenyekiti wa Bodi ya hospitali hiyo. Dr Wilbroad Peter
Slaa.
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii
wa Vodafone group, Andrew Dunnet akiwapiga picha kupitia simu yake ya mkononi
watoto wanaotibiwa katika Hospitali ya CCBRT Dar es Salaam wakati alipofanya
ukaguzi wa wodi za wagonjwa pamoja na Mabasi ya wagonjwa wa Fistula kabla ya
kukabidhiwa rasmi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho
Kikwete.
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii
wa Vodafone group, Andrew Dunnet akifurahi pamoja na watoto wanaotibiwa katika
Hospitali ya CCBRT Dar es Salaam wakati alipofanya ukaguzi wa wodi za wagonjwa
pamoja na Mabasi ya wagonjwa wa Fistula kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho
Kikwete.


Post a Comment