("fastjet"
au Kampuni”)
Mauzo ya
tiketi za fastjet yazinduliwa Tanzania
Nauli za
chini zaidi kuwahi kutokea kuna maana Watanzania wengi zaidi wanaweza
kupaa
13
Novemba 2012, Dar es Salaam - fastjet, Shirika la ndege la kwanza Afrika la
nauli nafuu, leo limezindua mauzo ya tiketi zake nchini Tanzania, ikiwa ni
maandalizi ya safari yake ya kwanza ya kibiashara mwishoni mwa mwezi
huu.
Uzinduzi
huo wa tiketi ni hatua muhimu katika juhudi za kampuni kuwezesha usafiri wa
ndege kwa Watanzania wako wengi ambao awali walikuwa hawamudu gharama za safari
za ndege. Huku nauli za anga zikiwa zinaanzia Tsh32, 000 (U$D20) kabla ya kodi
za serikali, usafiri wa anga sasa unakuwa moja ya njia nafuu za watu
kusafiri.
fastjet,
ambayo imeinunua Fly540, imechagua Dar es Salaam kuwa kituo chake cha kwanza cha
uendeshaji barani Afrika, huku safari za ndege zikiwa zimepangwa kuanza kuruka
kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuanzia Novemba 29. Tiketi
za Dar es Salaam – Kilimanjaro na Dar es Salaam – Mwanza zinaanza kuuzwa kuanzia
leo. Safari zingine, za ndani na kanda ya Mashariki mwa Afrika, zitaanza baada
ya wiki kadhaa.
Akizungumzia
uzinduzi wa mauzo ya tiketi, Afisa Mtendaji Mkuu wa fastjet, Ed Winters
alisema:
“Hiki ni
kipindi cha kihistoria kwa safari za anga Tanzania, na hasa Afrika. Usafiri wa
anga siyo tena himaya ya watu wachache Tanzania. fasyjet itafanya usafiri wa
anga kuwa kitu ambacho Watanzania wengi wanakimudu tofauti na awali, na hivyo
kutoa fursa nzuri zaidi kwa biashara, safari za likizo, na wanafamilia
kutembeleana. Tunawashukuru wabia wetu Tanzania kwa ushirikiano wao mpaka leo
hii, na tunamatumaini ya uhusiano mrefu na wenye manufaa kwa
watanzania.”
Tiketi
zinapatikana kupitia mawakala wa usafiri na dawati la mauzo, kituo cha
mawasiliano na ofisi za fastjet yenyewe. Tovuti mpya ya fastjet, www.fastjet,com
itazinduliwa wiki ijayo na kutoa taarifa za safari na nauli. Tovuti hiyo pia
itaruhusu kununua tiketi kwa kutumia kadi za credit/debit pamoja na simu za
mkononi.
Uzinduzi
wa Chapa ya fastjet
Fastjet
pia imezindua chapa yake mpya kabla ya kuanza kwa safari zake za kibiashara.
Nembo ya kampuni ni kasuku (kasuku wa kijivu wa Afrika) ambaye alichaguliwa
kutokana na sifa zake za maarifa, urafiki na kuakisi kaulimbiu ya fastjet ambayo
ni usafiri wa akili. Wiki hii pia itashuhudia uzinduzi wa mtandao wa kijamii wa
fsaftjet kupitia Facebook na Twitter na hivyo kutoa ukumbi kwa wateja na wadau
Kuwasiliana na kuchangia mawazo yao kuhusu kampuni kwa njia ya
mtandao.
Richard
Bodin, Afisa Biashara Mkuu wa fastjet anasema:
“Moja ya
hulka kuu za fastjet ni uwazi. Tunataka kuziba pengo kati ya mlaji na shirika la
ndege kwa kuhakikisha tunakuwa na mawasiliano ya pamoja kila inapowezekana na
kusikiliza mahitaji na vipaumbele vya wateja. Mitandao ya kijamii ni njia bora
ya kufanikisha hili – kumbi kama Facebook na Twitter hutuwezesha kuwasiliana
moja kwa moja na wateja na kutusaidia sisi kuelewa vizuri zaidi na kuiwezesha
fastjet kwenda sambamba na mahitaji na mapendeleo ya wadau
wetu.
Shirika
lina ndege tatu za kisasa aina ya Airbus A319. Ndege zote tatu zimo kwenye
mchakato wa kupakwa rangi na nembo za fastjet kabla ya kuletwa Tanzania tayari
kwa uzinduzi wa safari za kibiashara baadae mwezi huu.
MWISHO
Kwa
maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:
africapractice
Tanzania Tel: +255 (0)222 668 389
Teweli
Teweli
Meg
Muigai
Citigate
Dewe Rogerson, London Tel:+44 (0) 20 7638 9571
Angharad
Couch
Eleni
Menikou
TAARIFA
KWA WAHARIRI
Kuhusu
fastjet Plc
fastjet
Plc ni kampuni mama ya Shirika la Ndege la Afrika Fly540, ambalo hujiendesha
kutoka vituo vinne Kenya, Tanzania, Ghana na Angola. Kwa sasa Fly540 ina ndege
10 zenye kuhudumia kama njia 25 za ndani na kanda, ikibeba takriban abiria
750,000 kwa mwaka, huku ikiwa na msisitizo mkubwa kwenye usalama, ulinzi na
kuaminika.
Baada ya
mashauriano na mwanzilishi wa easyjet, Sir Stelios Haji-Ioannou, kampuni ya
easyGroup ililenga kubaini uwezekano wa kuwa na shirika la ndege la nauli nafuu
Afrika, kama ilivyo Ulaya, na hivi sasa tunajiandaa kuzindua fastjet, shirika la
kwanza la ndege Afrika la nauli nafuu, likiwa na ndege za kisasa kwa kutumia
leseni na njia za Fly540. Safari za kwanza kwa kutumia chapa ya fastjet
zinatarajiwa kuanza mwishoni mwa Novemba, na hivyo kuja na aina mpya kabisa ya
safari za anga kwenye soko la Afrika.
fastjet
Plc imeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la London (LSE). Kwa maelezo zaidi,
tembelea www.fastjet.com

Post a Comment