Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WADAU ZANZIBAR WAOMBWA KUCHANGIA SHULE ZA KATA TEMEKE DSM

Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya ‘Cooperation for assisting handicapped people’ inayojishughulisha na kusaidia watu wasiojiweza Mhina Michael Shengena akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Rahaleo Mjini Zanzibar kulia yake ni Mhariri Mkuu wa Maelezo Fakih Haji Mbarouk.

Wadau na Makampuni mbali mbali Zanzibar wameombwa kuichangia Taasisi ya ‘Cooperation for assisting handicapped people’ inayojishughulisha na kusaidia watu wasiojiweza ili Taasisi hiyo iweze kujenga Mabweni ya Shule mbili za kata Temeke Jijini Dar es Salaam.
Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo Mhina Michael Shengena wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Rahaleo Mjini Zanzibar.
Amesema wanahitaji wasaidiwe Sh Milioni Arobaini (40,000,000) ndani na nje ya Zanzibar kwa ajili ya ujenzi wa Mabweni ya watoto Yatima,Walemavu na Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ili waweze kupata taaluma ambayo itawasaidia katika maisha yao.
Amezitaja Shule ambazo wana mpango wa kujenga mabweni kwa wanafunzi hao kuwa ni Nguva na Sumangira zilizopo katika Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Aidha ametaja njia ambayo Wadau mbalimbali wanaweza kuchangia msaada wao kwa Kampuni hiyo kufanikisha ujenzi huo kuwa ni kupitia akauti namba 01J2070153800 ya CRDB Bank.
Mkurugenzi Mhina ameongeza kuwa watakuwa na ziara ya nchi nzima ambapo wanatarajia kukutana na Viongozi wa Serikali, Siasa, Dini na Wananchi mbali mbali katika kuitangaza Taasisi yao ili wadau waweze kuifahamu na kuichangia.
Aidha ametoa wito wa wananchi wa Zanzibar kushiriki katika harambee ya kuichangia Taasisi yao itakayofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani January 30, mwaka 2013 mjini Zanzibar.
Taasisi ya ‘Cooperation for assisting handicapped people’ yenye Makao Makuu yake Mkoani Iringa imesajiliwa mwaka 1998 chini ya Sheria za makampuni ya Tanzania Bara na kupewa namba za usajili 3388 ambapo shughuli yake kuu ni kusaidia watu wasiojiweza.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top