OGANAIZESHENI ya ngumi
za kulipwa Tanzania (TPBO) imetangaza kujitoa katika mpambano wa ngumi kati ya
mabondia Selemani Saidi na Caled Ameinda baada ya kudai muandaaji wa mpambano
huo ameshindwa kutimiza masharti kabla ya pambano hilo. Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Rais wa TPBO, Yassin Abdallah Mwaipaya kwa vyombo vya habari,
chama hicho kimeamua kujitoa baada ya kuona muandaaji wa pambano, Yusuph
Montanga (GACHA) anashindwa kutimiza masharti.
“Napenda kuwaarifu
kwamba TPBO haihusiki na pambano la ngumi za kulipwa kati ya mabondia waliotajwa
hapo juu. TPBO inalazimika kutoa taarifa hii kutokana na masharti iliyompatia
muandaaji wa pambano hilo GACHA kushindwa kuyatekeleza.
Pia izingatiwe kwamba
TPBO ilitoa kibali kwa muandaaji (GACHA) kwa ajili ya pambano kati ya bondia
THOMAS MASHALI VS SELEMANI SAIDI ambalo lilitakiwa kuchezwa katika uwanja wa
KINESI ulioko katika Jimbo la Ubungo Novemba 10, 2012.”
“…Lakini kokana na
kuumia kwa bondia THOMAS MASHALI katika pambano lake la kugombea ubingwa wa
AFRIKA MASHARIKI NA KATI dhidi ya bondia kutoka uganda MEDI SEBYALA, tpbo
ililazimika kumsaidia muandaaji huyo ndg GACHA ili aweze kumpata bondia kutoka
kenya ili awe mbqdala wa THOMAS MASHALI,” alisema Mwaipaya katika taarifa
yake.
Akielezea zaidi Mwaipaya
alisema; “…TPBO ilianza mawasiliano na kocha Juliusn Odhiambo kutoka Kenya ili
atupatie bondia wake. Lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele TPBO ilipata
wasiwasi na uwezo wa muandaaji huyo kuweza kuandaa pambano hilo hasa alipofikia
kutopokea simu ya RAIS wa TPBO kuhusu maendeleo ya maandalizi ya pamnao
hilo.
“Novemba 5, 2012
nilimuagiza ndg GACHA alete pesa za kuwasafirisha bondia na kocha wake kutoka
kenya ili wawasili nchini siku ya alhamisi usiku kwa ajili ya zoezi la upimaji
wa uzito siku ya ijumaa kwa ajili ya pambano la Novemba 10, 2012 kama kanuni ya
ngumi za kulipwa zinavyoamuru, upimaji wa uzito kwa mabondia siku moja kabla ya
pambano.”
“Na ikafikia hata mimi
kumpatia GACHA namba za simu za ndg bakari ambaye ni mfanyakazi wa SPIDER BUS
SERVISES ili awasiliane naye kuhusu ujio huo wa bondia kutoka kenya. lkn mpaka
hivi sasa ninapoandika taarifa hii kwenu sijapata taarifa yoyote inayohusu
kuwasili kwa mabondia hao kutoka kenya na hivyo TPBO haiwezi kuvnja kanun i za
mchezo wa ngumi za kulipwa, kwa kumfurahisha tu MUANDAAJI.”
TPBO pia ilimpa masharti
GACHA awasilishe TPBO pesa za kuwarudisha wakenya baada ya mchezo badala ya
kutegemea makusanyo ya mlangoni, pia awasilishe DOLA 100 ambayo ilikuwa ni
malipo ya bondia huyo kutoka kenya kabla ya pambano, lakini alikataa. Kwa
taarifa hii TPBO inatamka rasmi kwamba isihusishwe na lolote litakalotokea
endapo bondia huyo kutoka kenya atakuwa amewasili kwa njia zingine ambazo NDG
GACHA atakuwa ameamuwa kuzitumia.
TPBO inalazimika kutowa
taarifa hii kwenu ili kulinda heshima yake na uaminifu ambayo imejijengea katika
nchi nzima ya tanzania na haiko tayari kufanya kazi na waandaaji ambao uwezo wao
ni wa kujaribu jaribu mambo na siyo wazoefu kwani hatimaye huwa ni kuuvunjia
heshima mchezo wa ngumi za kulipwa na kusababisha udharauliwe.
Wakati TPBO ikijitoa
katika pambano hilo, maandalizi ya mpambano kati ya mabondia hao yaani SELEMANI
SAIDI na CALED AMAEINDA yanaendelea na pambano linatarajia kuchezwa kesho katika
uwanja wa KINESI ulioko Ubungo. Akizungumza na vyombo vya habari Rais wa PST,
Emanuel Mlundwa amethibitisha kuwepo kwa mpambano huo ambapo CALED AMAEINDA wa
Kenya tayari amewasili kwa ajili ya mpambano na Seleman siku
iliyopangwa.
Alisema taarifa
zilizotolewa na TPBO imewakera hivyo wao kuamua kuingilia kuchukua jukumu la
kukwamua ili kufanyika mpambano huo na lengo kubwa ni kuhakikisha mabondia
wapate ridhiki yao ya alali kama walivyokubaliana katika mkataba. Mlundwa
alisema mabondia ndio wanaopigana hivyo hana sababu ya kusitisha mpambano huo
kwa baadhi ya watu wachache wasioutakia mema mchezo wa masumbwi kuleta fujo za
uongozi wa hapa na pale.
Mpambano huo utakuwepo
pale pale kesho kuanzia saa kumi jioni na kuendeklea na baadhi ya wachezaji
wanaocheza utangulizi wamepima uzito leo kwa ajili ya mpambano huo na kuwataka
mashabiki kujitokeza kwa wingi kuangalia masumbwi hayo
Post a Comment