Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Tume ya Katiba yaingia Dar, Arusha

TUME ya Mabadiliko ya Katiba, inatarajia kuendelea na awamu ya nne na ya mwisho ya mikutano yake na wananchi wa mikoa sita kuanzia Novemba 19 hadi Desemba 19 mwaka huu, kwa lengo la kukusanya maoni ya wananchi.
Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Arusha, Simiyu, Geita, Mara na Mjini Magharibi ambapo kila siku kutafanyika mikutano miwili, wa kwanza utaanza saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana na mwingine saa 8:00 alasiri hadi saa 11:00 jioni.
Taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari jana na Katibu wa Tume hiyo, Assaa Rashid, ilisema kuwa taratibu zote za kuanza kazi ya kukusanya maoni katika mikoa hiyo zimekamilika.
Alisema kuwa wajumbe wa tume na watumishi wa sekretarieti wamejigawa katika makundi saba, ambapo kila mkoa utakuwa na kundi moja isipokuwa Dar es Salaam itakayokuwa na makundi mawili.
“Kwa Dar es Salaam tume imejigawa katika makundi mawili na siku hiyo itaanza na wilaya za Temeke na Ilala. Katika Wilaya ya Temeke, itaanza na eneo la Keko wakati katika Wilaya ya Ilala itaanza na eneo la Jangwani,” alisema.
Mkoani Arusha, tume itaanza na Wilaya ya Karatu eneo la Mbulumbulu wakati mkoani Mara itaanza katika Wilaya ya Tarime eneo la Bumera na mkoani Simiyu, itaanza na Wilaya ya Busega eneo la Lamadi.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa mkoani Geita, tume itaanza na Wilaya ya Chato eneo la Kachwamba huku Mkoa wa Mjini Magharibi, itaanza katika Wilaya ya Magharibi.
Kwamba, pamoja na kuwasilisha maoni kupitia mikutano itakayoitishwa na tume, wananchi pia wanaweza kuwasilisha maoni yao kupitia tovuti ya tume (www.katiba.go.tz) au kwa njia ya posta.
Alisema anuani zifuatazo zinaweza kutumika, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Makao Makuu, Mtaa wa Ohio, S.L.P. 1681, Dar es Salaam, simu: +255 22 2133425, nukushi: +255 22 2133442.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top