Jengo la
Bunge la Marekani, Washington DC
UCHAGUZI
mkuu Marekani umemalizika huku kukiwa na mabadiliko kiasi ya viti vya bunge,
uwiano wa madaraka kati ya baraza la Seneti na bunge unabaki kuwa vile
vile.
Katika baraza la seneti chama cha Democrat
kimeongeza angalau kiti kimoja na chama cha Republican kimepoteza kiti kimoja,
hii ikimaanisha kuwa baraza la seneti mwaka 2013 litakuwa na wademocrat
wasiopungua 51, wa-Republicans wasiopungua 44 na angalau viti viwili vya wabunge
wa kujitegemea.
Viti vitatu bado havijajulikana vitakuwa
vinaegemea chama gani.
Akizungumza na Sauti ya Amerika, Professa Julius
Nyang’oro wa chuko kikuu cha North Carolina alisema Wademocrat wamepiga hatua
kubwa katika baraza la seneti ambapo jimbo la Massachusetts, m-Democrat
Elizabeth Warren alimshinda Seneta wa sasa Scott Brown kutoka chama cha
Republican.
Chama cha Democrat kimechukua ushindi pia
katika jimbo la Virginia lenye upinzani mkali, ambapo gavana wa zamani wa
Democrat Tim Kaine alimshinda gavana wa zamani wa Republican, George Allen
Post a Comment