Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UCHAWI ULIPOBISHA HODI NYUMBANI KWA KHADIJA KOPA

HARAKATI za uchaguzi zina mambo! Wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Magomeni, Bagamoyo uliofanyika hivi karibuni, kulikuwa na vituko kibao moja wapo ni ile ya imani za kishirikina.
Mgombea wa kiti hicho kwa upande wa Chama tawala (CCM), Jafari Ali Yusuf ambaye ni mume wa Malkia wa mipasho, Khadija Kopa alikumbana na vituko vya ushirikina.
Katika moja ya vyumba vya nyumba yao hapo mjini Bagamoyo, kulikutwa Paka aliyekufa sambamba na vikorokoro vingine vinavyoashiria mambo ya kishirikina. www.saluti5.com ilikuwepo na ikashuhudia kihoja hicho.
Lilikuwa jambo liliowaduwaza wengi, haikujulikana paka huyu aliingizwa vipi wakati nyumba nzima ilikuwa imefungwa.
Licha ya wenye nyumba (Kopa na mumewe) kupuuzia jambo hilo lakini wapambe wao walionyesha kila dalili ya kuamini kuwa huo ni ushirikina uliotumwa na aidha wapinzani wao au watu wasiowatakia mema katika harakati zao za kisiasa.
Katika uchaguzi huo, Jafar Ali alishinda kwa kishindo na kutawazwa kuwa Diwani mpya wa kata ya Magomeni
 
Chanzo: saluti5.com
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top