KWA mwaka huu wa 2012 kuna mambo mengi yamepita na kusisimua ikiwa pamoja na majozi baada ya kuondokewa na nyota katika tasnia ya filamu lakini pia sherehe za kihistoria na matumizi ya fedha za kutisha kama si kutanua pia yalitokea maradhi yaliwapata pia wanatasnia ya filamu na kuhitaji msaada uliozua mjadala na kuonyesha jinsi tasnia hiyo ilivyo ngumu isiyo na Bima kwa wasanii.
Lakini leo pamoja na hayo kuna matukio mawili ya yanayowahusu wasanii wa kike ambao FC kwa utafiti inajaribu kuwaangazia macho ya karibu ya wasanii hawa yaani Aunty Ezekiel na Jaqueline Wolper baada ya kutawala vichwa vya habari katika vyombo vya habari mbalimbali wakionyesha jeuri ya fedha na kuwakoga wasanii wenzao.
Siku za nyuma Jack alishika vyombo vya habari akiwa ndio msanii wa kike mwenye kumiliki magari ya thamani huku akitanua na kutangaza kubadili dini kwa ajili ya kuolewa na jamaa alijulikana kwa jina la Dalas ambaye inasemekana alikuwa ughabuni katika kutafuta Ngawila ili akirudi Bongo maisha yaendelee lakini siku ya siku ikabaki hadithi.
Hatutakia kuingia ndani sana lakini hiyo ni sehemu ya maisha ya nyota wetu kwa sasa fedha zao hazitokani na filamu bali nje ya fani hiyo sijui tuite ni wafadhili au mapedejee bali ukweli utaendelea kubaki pale pale akina dada katika tasnia ya filamu wanatafuta fedha kwa nguvu zao zote katika kulinda hadhi ambayo pengine haipo.
Hivi karibuni mwanadada mwenye fani ya ulimbwende Aunty Ezekiel Jujuman alitikisa uwanda wa tasnia ya filamu pale alipofanya matukio ya kuandika historia alipoandaa sherehe za kuagwa kuanzia Kitchen party na hatimaye Sendoff katika Hotel ya kimataifa ya Serena baada ya ndoa yake kufungwa katika staili ya aina yake ndoa ilifungwa kwa niaba ya muoaji.
Mjini kuna mengi yanaongelewa kuhusu tukio hilo au jeuri ya fedha ilivyofanyika kwa nyota hawa kwa mwaka 2012, kuna wale wanaodai kuwa wasanii wamejikuta wakifanya mambo makubwa kwa ajili ya muonekano tu huku wakiamini kuwa sehemu kubwa ya uhusiano unaotangazwa umezingirwa na ubatili wa ndoa hizo kwani pamoja na wasanii hao kubadili Dini zao za asili mwisho wake unashangaza.
Lakini pamoja na hayo yanayozungumzwa watafiti wa mambo yanayotawliwa na utata wanajiuliza kuwa baada ya kupita mwaka huu kati ya Aunty na Jack Wolper nani atakumbukwa iwe kwa wasanii au wapenzi wa filamu Swahiliwood?
.
.
Baada ya kutangaza uchumba na Dallas Jack alipata safari kwenda nje na kurudi wakiwa nchi mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Bongo Juma Kilowoko ‘Sajuki’ maradhi yaliyohitaji fedha nyingi kwenda kutibwa nchini India Jack Wolper aliguswa na kutoa Dola 16,000/ ndiye msanii pekee wa filamu kutoa fedha nyingi kumsaidia msanii mwenzake Tanzania haijawahi kutokea anastahili kupongezwa.
Ukija kwa dada yangu Aunty naye akiwa mfanyabiashara anayemiliki Grocery maarufu sehemu za Mwananyamala katika matukio ya kuandika Historia aliwakusanya nyota na watu wa kawaida katika Hoteli ya kimataifa ya Serena na waarikwa kula Bata huku wakifurahia na kupiga picha za kumbukumbu.
Hayo ndio maisha ya wasanii wa Bongo kwa mfano Aunty pia akiwa na mlimbwende mwenzake Wema Sepetu nao walikuwa na yao katika majukwaa kuvaa vinguo vifupi na kuzua mjadala Bongo siku ya siku wakaomba msamaha wenye utata hiyo ndio Bongo movie film.
IMETOKA www.filamucentral.co.tz
Post a Comment