Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii
Tanzania TTB Devotha Mdachi akizungumza na Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa
Uingereza na Mbunge wa Jimbo la South Shields Mh.David Miliband wakati ujumbe wa
TTB ulipotembelea Uwanja wa Sunderland FC na kushuhudia mchezo wa ligi kuu ya
Uingereza kati ya timu hiyo na timu ya Aston Villa uliofanyika siku ya jumamosi
nchini Uingereza, Bodi ya utalii Tanzania inatangaza matangazo ya utalii wa
Tanzania katika viwanja sita vinavyotumika kuchezea ligi kuu ya Uingereza
(Premier Liegue) kikiwemo kiwanja cha Sunderland FC, katika picha katikati ni
Edmund Hazal Mkurugenzi wa Kampuni ya Lantech Services inayoratibu matangazo
hayo,Bw. David Miliband pia ni mwenyekti wa klabu ya Sunderland. (Picha na
www.fullshangweblog.com).
Waziri wa mambo ya nje wa
zamani wa Uingereza na Mbunge wa Jimbo la South Shields Mh.David Miliband akiwa
katika picha ya pamoja na Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw.
Geofrey Meena kushoto mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu ya
Uingereza kati ya Suderland na Aston Villa, David Miliband pia ni mwenyekiti wa
klabu ya Suderland
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya
UtaliiTanzania TTB Devotha Mdachi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa
zamani na maafisa wa timu ya Sunderland FC baada ya kukabidhiwa zawadi ya saa
kutoka kulia ni Balozi wa Sunderland na Golikipa wa zamani Jimmy Montgomery,
Gary Mutchinson Mkurugenzi wa Biashara na Kevin Ball Nahodha wa zamani wa timu
hiyo.
Balozi wa Sunderland na Golikipa wa zamani
Jimmy Montgomery kiutambulisha ujumbe wmaafisa wa bodi ya utalii TTB
ulipotembelea uwanja huo.
Ujumbe wa bodi ya Utalii Tanzania
ukishuhudia mchezo huo.
Ujumbe wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB
akipiga picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Sunderland katika hafla hiyo wa
pili kutoka kulia waliosimama nyuma ni James MacFadden wa nne ni David Meyler na
wa sita ni Titus Brambie.
Hapa ndiyo lango kuu la kuingilia kwenye
jukwaa kuu la uwanja huo
Ujumbe wa Bodi ya Utalii na
maafisa wa taasisi mbalimbali wakipiga picha ya pamoja nje ya uwanja huo kutoka
kulia ni Bw. Manase kutoka Ngorongoro, Bw. Mukhtar kutoka Jumuiya ya Afrika
Mashariki , Mkurugenzi wa Masoko TTB Devotha Mdachi, Geofrey Meena Meneja Masoko
TTB na Edmond Hazal Mkurugenzi wa kampuni ya Lantech Services inayoratibu
matangazo hayo katika viwanja vya ligi kuu Uingereza.
Ujumbe wa Bodi ya Utalii ukiwa
katika picha ya pamoja na mwenyeji wao Mkurugenzi wa Biashara wa Sport Five Tony
Davison.
Hapa ujumbe huo ukipata maelezo
kwenye uwanja wa Sundrland FC kutoka kwa Tour Guide Gerad
Cronin
Kutoka kulia ni Bw. Manase,
Geofrey Meena, Mukhtar na Devotha Mdachi wakiwa wamekaa katika moja ya maeneo ya
benchi la ufundi uwanjani hapo.
Meneja masoko wa Bodo ya Utalii
akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi hiyo Devotha Mdachi wakati
walipotembelea uwanjani hapo jumamosi iliyopita , katikati ni Bw. Mukhtar wa
(EAC) nBw. Manase kutoka hifadhi Ngorongoro.
Hapa wakielekea katika eneo
maalum la migahawa na baa uwanjani hapo.
Mashabiki wa timu hiyo wakiwa
wamefurika uwanjani hapo ili kushuhudia mpambano huo.
Wachezaji wa timu ya Sunderland FC
wakilianzisha dimba
Hapa wanakosa
goli.
Kutoka kulia ni Tony Davison,
Geofrey Meena, Edmond Hazal na Devotha Mdachi wakifurahia jambo wakati mchezo
huo ukiendelea kati ya Sunderland na Aston Villa.
Matangazo ya Utalii wa Tanzania yakipita
katika lininga maalum za matangazo uwanjani hapo kama
yanavyoonekana.
Matangazo ya Utalii wa Tanzania
yakipita katika lininga maalum za matangazo uwanjani hapo kama
yanavyoonekana.
Hapa wakigonganisha glasi kutoka kulia ni
Geofrey Meena, Devotha Mdachi, Tony Davison na Moses
Mwangi.
Wanachama matajiri mbalimbali
wa timu ya Sunderland FC wakiwa katika hafla hiyo katika moja ya migahawa, baa
na kumbi kubwa zilizopo uwanjani hapo.
on Monday, November 5, 2012
Post a Comment