KATIKA kuhakikisha ari ya wachezaji inarudi kama
ilivyokuwa mwanzo, uongozi wa klabu ya Simba una mpango wa kuipeleka timu nje ya
nchi ili kuwapa muda wachezaji wa kusahau yaliyopita na kujipanga vema kwa
mzunguko wa pili.
Aidha, uongozi wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya
Vodacom, umemuomba radhi kipa na nahodha wake, Juma Kaseja kutokana na
kudhalilishwa na baadhi ya watu baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo usioridhisha
katika michezo yake ya mwishoni mwa mzunguko wa kwanza.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amesema leo kwamba
kudhalilishwa kwa Kaseja si sahihi kwani anaweza kukofanya makosa ya kiufundi
kama binadamu mwingine, hivyo anahitaji ushauri wa kimawazo.
“Tuache kudhalilisha
wachezaji kwani kufanya hivyo si uungwana wa michezo hata kidogo…kila mtu
anafahamu kuna kushinda, kufungwa na kutoka sare, kama hatutaki kufungwa
tujiondoe wenye ligi,”alisema Rage
Post a Comment