Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jana, Mwenyekiti wa UVCCM, Sadifa Hamis Juma alisema kuna baadhi ya vigogo wenye malengo ya kuwania nafasi ya urais wanawagawa vijana.
Mkutano huo ulihudhuriwa na vigogo wa chama hicho akiwamo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na baadhi ya mawaziri.
UVCCM wamekuwa wakituhumiwa kutumiwa na vigogo walio katika mbio za kuwania urais mwaka 2015.
UVCCM wamekuwa wakituhumiwa kutumiwa na vigogo walio katika mbio za kuwania urais mwaka 2015.
Wakati wa uchaguzi wa ndani wa chama hicho, imekuwa ikielezwa kuna wagombea urais waliokuwa wakihaha kuhakikisha nafasi za uongozi wa jumuiya hiyo zinachukuliwa na vijana wanaowaunga mkono. Sadifa alisema makundi yaliyokuwapo kabla na baada ya uchaguzi wa jumuiya hiyo, sasa yanatakiwa kuvunjwa na kujenga umoja huo kwa masilahi ya chama.
Alisema kitendo cha wanaotaka urais kuwatumia vijana kama ngazi, sasa watambue kuwa hawapo tayari kwa hilo.
Chanzo: Mwananchi
Chanzo: Mwananchi
Post a Comment