TAARIFA KWA
UMMA
Wizara ya Nishati na Madini (MEM)
inapenda kuutangazia umma kuwa Serikali inatarajia kuzindua mradi
wa ujenzi wa miundombinu ya kusafisha na kusafirisha gesi asilia kutoka Mnazi
Bay Mtwara na Songo Songo Kilwa hadi Dar es
Salaam.
Hafla ya kuweka Jiwe la Msingi wa
mradi huo itafanyika tarehe 8/11/2012 Kinyerezi, Manispaa ya
Ilala, katika eneo ambapo mitambo ya kuendeshea mfumo mzima wa gesi itajengwa.
Mgeni rasmi katika sherehe hiyo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Wananchi wote wa Dar es Salaam na
maeneo yanayozunguka eneo la Kinyerezi mnaalikwa na mnaombwa kufika kwenye eneo
la mradi saa 2.00 asubuhi.
GESI ASILIA KWA MAENDELEO YA
TAIFA
Imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini
Post a Comment