Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Uzinduzi Wa Sultan ‘Qaabos Academic Fellowship’- SUZA


 


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imezindua Mpango wa maendeleo ya elimu ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) unaofadhiliwa na Sultan Qaboos bin Said wa Oman ujulikanao kwa jina la Sultan Qaboos Academic Fellowship (SQAF) na unatarajiwa kuanza rasmi shughuli zake mwaka ujao wa masomo 2014-2015 ambapo wazanzibari 50 watafaidika kila mwaka.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali juma Shamhuna ameuzindua mpango huo katika sherehe zilizofanyika Kempasi mpya Tunguu kilomita kumi kutoka mjini Unguja na amesema SUZA ndio Chuo pekee cha Serikali kilichopewa jukumu la kukuza elimu hivyo suala la kuwatafutia wananchi vyuo ndani na nje ya nchi litaendelea.

Amesema Wizara ya Elimu itaendelea kushirikiana na SUZA na Vyuo vyengine vya Elimu ya juu katika kuwashajiisha wananchi wenye sifa kupata fursa ya masomo kupitia mpango huo wa SQAF.

Amewahakikishia wananchi kwamba mfuko huo hautakuwa na ubaguzi wa aiana yoyote na hautaangalia itikadi ya chama wala jinsia na watu wenye ulemavu pia wanayonafasi kubwa zaidi iwapo wataomba, muhimu ni kuwa na sifa zinazokubalika.

Amesema kutaundwa kamati ya wajumbe sita, watatu kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar na watatu kutoka Oman kushughulikia majina ya watu watakaoomba masomo nchi mbali mbali na kamati hiyo ndio itakuwa na jukumu la kuteua majina watakaoingia vyuoni kwa mujibu wa vigenzo na sifa zao.

Hata hivyo amesema wafanyakazi wa SUZA watakaoomba watapewa kipaumbele kupitia mpango huo lakini wafanyakazi wa vyuo vyengine vya elimu ya juu na ambao bado hawaja ajiriwa sehemu yeyote lakini wanazo sifa wataruhusiwa kuomba.

Waziri Shamhuna amemshukuru Mfalme Qaboos kwa kukubali kusaidia maendeleo ya Elimu Zanzibar na amemuhakikishia kwamba Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar itasimamia kwa ufanisi mkubwa mpango huo ili kuona unaleta tija kwa wananchi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkamu Mkuu wa Chuo cha SUZA Professa Idrissa Ahmad Rai amesema lengo la mpango wa Sultan Cabos Academic Fellowship for SUZA
ni kuwajengea uwezo katika rasilimali watu utakaokuwa na wataalamu watakaomudu kuleta maendeleo, utangamano na ustawi bora wa uchumi wa Zanzibar.

Amesema kufanikiwa kwa mpango huo kutatimiza matarajio mema ya Sultan Qaboos Bin Said wa Oman na DK. Ali Mohd Shein, Rais wa Zanzibar na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kujenga amani na mustakabali mwema wa elimu Zanzibar.

Ameongeza kuwa kutakuwa na aina tatu za wanafunzi wenye sifa ambao wataweza kuomba nafasi za masomo kupitia mpango SQAF ambazo ni waajiriwa wa SUZA, wasiokuwa waajiriwa wa SUZA lakini watapatiwa Ufadhili wa mpango huo lakini watafanya kazi SUZA baada ya kumaliza masomo yao na waombaji makini kutoka taasisi nyingine watakao onyesha uwezo na utayari wa hali ya juu.

Amesema katika mpango wa SQAF hakutakuwa na upendeleo wa aina yeyote na watu watakaochaguliwa itawalazimu kufanya mitihani ya kiingereza na kupasi na hilo ni miongoni mwa sifa za kupata ufadhili.

Mpango wa Sultan Cabos Academic Fellowship for SUZA utadhamini masomo kuanzia shahada ya pili na kuendelea katika vyuo mbali mbali vya Ulaya. Asia. Marekani na vyuo vyengine duniani kote kulingana na masomo husika.
mwisho
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top