UTAPELI wa aina
yake, umeibuka mkoani Kilimanjaro ambapo kundi la matapeli hula njama na
wanawake kuandaa mitego ya fumanizi na kujipatia mamilioni ya shilingi.
Uchunguzi wa kina
wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa kundi hilo limekuwa likiwalenga wanaume
walio katika ndoa na wenye uwezo wa kifedha, ambao baada ya kunaswa katika
fumanizi hizo hupigwa picha zinazogeuzwa mradi.
Utapeli huo
unawalenga wafanyabiashara, watu wenye nyadhifa kwenye taasisi na hata viongozi
wa dini.
Kundi hilo lenye
mtandao mpana nchini, linaonekana katika siku za karibuni kujikita katika mkoa
wa Kilimanjaro.
Uchunguzi huo
unaonyesha kuwa katika kipindi cha wiki mbili, watu wanne wamejikuta wakinaswa
katika mtego huo na kutoa kitita cha kati ya Sh3 milioni na Sh10 milioni,
gharama hizo zikiwa nje ya zile za kukomboa picha.
“Kwa hofu ya taarifa kumfikia mkewe, jamaa yangu aliamua kutoa fedha walizotaka, na unajua unapofumaniwa akili zinapotea kwa muda na unakuwa huna ujanja,” kilidokeza chanzo chetu.
“Kwa hofu ya taarifa kumfikia mkewe, jamaa yangu aliamua kutoa fedha walizotaka, na unajua unapofumaniwa akili zinapotea kwa muda na unakuwa huna ujanja,” kilidokeza chanzo chetu.
(Kundi hilo hufanya kazi kwa kuwatumia wasichana
wadogo na wakubwa, ambao wanaajiriwa maalumu kwa kazi hiyo ambayo haitofautiani
na ya uchangudoa).
Mbali na waume za
watu, wengine ambao wamenaswa kwenye mtego huo ni baadhi ya mapadri wa Kanisa
Katoliki, ambao hulazimika ‘kumalizana’ nao wakihofia kuchafuliwa kwa kashfa
iwapo jambo hilo litaanikwa kwa umma.
Katika tukio la
hivi karibuni, mfanyabiashara mmoja wa mjini Moshi alinaswa katika fumanizi hilo
na mwanamke mmoja aliyedaiwa ni mkazi wa eneo la KDC Barabara Kuu ya Moshi-Himo
na kulipa Sh3 milioni.
“Kwa hofu ya
taarifa kumfikia mkewe, jamaa yangu aliamua kutoa fedha walizotaka, na unajua
unapofumaniwa akili zinapotea kwa muda na unakuwa huna ujanja,” kilidokeza
chanzo chetu.
Hata hivyo,
chanzo hicho kilidai kuwa baada ya kupita wiki moja, mfanyabiashara huyo
alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mwandishi wa gazeti moja la
udaku akimtaarifu kuwa ana picha za mfanyabiashara huyo alizopigwa kwenye
fumanizi.
“Baada ya hapo
tuliifuatilia namba yake na tumegundua anaitwa (jina tunalo), lakini kule kwenye
lile gazeti hawamfahamu kabisa wala hiyo namba hawaijui,” alidai ndugu wa
mfanyabiashara huyo.
Alidai kuwa,
baada ya kumfuatilia mwanamke anayedaiwa kufumaniwa na ndugu yao, waligundua pia
kwamba, tukio hilo ulikuwa ni mchezo mchafu.
Post a Comment