GEITA, TANZANIA
Baada ya Naibu Waziri Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri, kuagiza waliohusika na
upotevu wa sh. milioni 16.6, za Halmashauri ya Kijiji cha Katoro mkoani Geita,
wakamatwe haraka na kufikishwa mahakamani, viongozi watatu wa kijiji hicho,
akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji, Joel Mazemule (CHADEMA), wamekamatwa na
walitarajiwa kufikishwa mahakamni leo kuhusiana na upotevu wa fedha hizo.
Mwanri alitoa agizo hilo wakati
wa ziara ya Sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa, iliyongozwa na
Katibu Mkuu wa Chama, Abdulrahman Kinana, baada ya wananchi kuelezwa kuwa,
viongozi hao wametafuna kiasi hicho cha fedha lakini hakuna hatua
zilizochukuliwa dhidi yao.
Kamanda
wa polisi Mkoani Geita, Leonard Paulo, katika taarifa yake kwa waandishi wa
habari jana, aliwataja watuhumiwa wengine waliokamatwa pamoja na Mazemule (42)
kuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Katoro, Fundi Makanza(44) na kuwa mwingine ni
Mjumbe wa serikali ya kijiji hicho kupitia CHADEMA, Charles Malegi (34).
Kamanda
huyo alisema “Ni kweli tunawashikilia hawa viongozi watatu toka jana kwa tuhuma
za ubadhilifu wa sh. Milioni 116.6 ambazo ni mali ya umma.”
Alieleza
kwamba, polisi limefuatilia vielelezo vyote ikiwemo nakala halisi zilizotolewa
na Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Alexander Lumelezi na
kujiridhisha, ndio maana wakawakamata.
Alisema,
fedha hizo zinazodaiwa kutafunwa na watuhumiwa hao, zilitokana na ukusanyaji
ushuru, toka katika vyanzo mbalimbali vikiwemo mashamba, visima na maduka
yaliyopo kijijini hapo.
Alifafanua
kuwa, kati ya mwaka 2010/2011 kiasi kilichokusanywa na watuhumiwa hao kilikuwa
sh. mil 21.3 lakini sh. Milioni l6.6 zilipotea na hadi sasa hazijulikani
zilipokwenda.
Kamanda
Paul alisema, watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kujibu
tuhuma zinazowakabili.
Post a Comment