Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe
amempokea na kumkaribisha Waziri wa Maji Mhe. Jumanne Maghembe na ujumbe
wake kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) katika
Ofisi za Ubalozi hapa nchini Uingereza. Mheshimiwa Maghembe na ujumbe
wake uko nchini Uingereza kwa ziara rasmi ya kikazi na ya kiserikali. Ujumbe
huo, ukiongozwa na Mhe. Maghembe, utapata fursa ya kutembelea Makampuni,
Taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi zinazoshughulika na utoaji wa
huduma ya Nishati na Maji hapa Uingereza, vilevile Ujumbe
huo utafanya majadiliano na Viongozi Wakuu katika Sekta hiyo ya Nishati na
Maji kwa nia ya kupata ushauri wa Kitaalam wa kutafuta njia zaidi za kuboresha
utoaji wa huduma hizo nchini kwetu Tanzania.
Mheshimiwa Balozi Kallaghe, alitumia fursa hiyo kumfahamisha
Mhe. Waziri Maghembe maendeleo ya kazi za Diplomasia ambazo Ubalozi unafanya
kwa niaba ya serikali nchini Uingereza. Kwa upande wake Mheshimiwa Waziri
Maghembe, alielezea mafanikio ya serikali katika kuwapatia wananchi huduma ya
maji na juhudi zinazoendelea kufanywa kuondoa tatizo la Maji na kuhakikisha
tatizo hilo linakuwa historia nchini Tanzania.
Waziri Maghembe anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo
na viongozi wakuu wa sekta ya Nishati na Maji nchini Uingereza yenye lengo la .
Aidha ujumbe huo wa Tanzania, ukiongozwa na Mheshimiwa Waziri Maghembe
utamaliza ziara yake nchini Uingereza siku ya Alhamis, tarehe 29 Novemba 2012.
Mheshimiwa Waziri Maghembe, pamoja na Mheshimiwa Balozi
Kallaghe, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa kutoka Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na baadhi ya Maofisa wa Ubalozi
hapa London.
Post a Comment