Wabunge wa
Somalia
Bunge nchini Somalia
limeidhinisha baraza jipya la mawaziri kumi waliloteuliwa na waziri mkuu Abdi
Farah Shirdon. Wanawake wawili ni miongoni mwa walioteuliwa.
Serikali kwa mara ya
kwanza ina waziri wa kwanza mwanamke atakayeshikilia wadhifa wa waziri wa mambo
ya nje, Fauzia Yusuf Haji Adan na ambaye anatoka Somaliland.
"Wabunge walipitisha
baraza hilo kwa kura 219 , kati ya wabunge 225, waliohuduhuria kikao'' alisema
spika wa bunge Mohamed Osman Jawari.Kuidhinishwa kwa baraza hilo kumekuja licha
ya ripoti kuwa baadhi ya koo hazikuwakilishwa vyema kwenye baraza hilo
liliotajwa wiki moja iliyopita.
Wabunge watatu
waliwakataa mawaziri hao huku wengine watatu wakijizuia kupiga
kura.''
Rais mpya pamoja na
wabunge wapya walichaguliwa hivi karibuni nchini Somalia , nchi iliyokuwa haina
serikali thabiti kwa zaidi ya miaka 20.
Serikali mpya
inakabiliwa na changamoto nyingi wakati ikijaribu kuleta utulivu na utahbiti
katika nchi hiyo ambayo imekumbwa na vita vya muda mrefu pamoja na tisho la
wanamgambo wa Al Shabaab ambao wametishia kuipindua wakisema inaungwa mkono na
nchi za Magharibi.


Post a Comment