Mwenyekiti na
Mwanzilishi wa East African Speakers Bureau Limited (EASB) Paul Mashauri
akizungumzia umuhimu wa kukuza mtandao wa vijana wajasirimali nchini ili kupanua
wigo wa mawasiliano miongoni mwao katika moja ya njia ya kukuza vipaji na
mawasiliano ya kirafiki.
Chief Technical Advisor
Youth Entrepreneurship Facility and WED -ILO Bw. Jealous Chirove akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Kimataifa ya Wajasiriamali uliofanyika jijini Dar
es Salaam ambapo amesema vijana lazima wawe na moyo wa kujituma na kuhakikisha
wanapanua wigo wa kujiajiri wenyewe na kuondokana na fikra za kuajiriwa peke
yake.
Aliongeza kuwa
ujasiriamali katika nchini kama Tanzania ni mkombozi wa pekee katika tatizo la
ajira hasa kwa vijana kwa kujiendeleza na mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali
kama njia pekee ya kujiajiri wenyewe.
Mwenyekiti wa Shirika
Lisilo la Kiserikali la ZAYEE (Zanzibar Association for Youth Education and
Empowerment) Bw. Masoud Salim Mohamed ambao ndio waandaaji wa maadhimisho ya
wiki ya wajasiriamali inayoendea jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Shirika
Lisilo la Kiserikali la ZAYEE (Zanzibar Association for Youth Education and
Empowerment) Fatma Mabrouk Khamis akielezea jinsi alivyovutiwa kufanya
maadhimisho ya Wiki ya Kimataifa ya Wajasiriamali hapa Tanzania ikiwa ni mara ya
kwanza baada ya kuona yanavyofanyika nchini Marekani alikokwenda kujifunza juu
ya ujasiriamali.
Mratibu Kitaifa Mradi wa
Maendeleo ya Ujasiriamali kwa Wanawake (WED) Bi. Noreen Toroka akitoa changamoto
kwa mabinti waliohudhuria semina hiyo kutokuwa na uwoga wa kuchangia mada na
kuuliza maswali na vile vile kujiamini pia.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Professional Approach Group Modesta Mahiga akitoa nasaha zake kwa vijana
mbalimbali kuhusu ujasiriamali faida na changamoto zake wakati wa maadhimisho ya
wiki ya ujasiriamali hapa nchini.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Relim Entertaiment, Bi. Emelda Mwamanga Mtunga akizungumza wakati wa maadhimisho
ya wiki ya ujasiriamali ambapo alitumia nafasi hiyo kuelezea uzoefu na
changamoto za ujasirimali nchini.
Mshehereshaji wa Wiki ya
Kimataifa ya Wajasiriamali (GEW) Bw. Austin Makani akitambulisha baadhi ya
Wafanyakazi wa ILO (hawapo pichani).
Baadhi ya Wafanyakazi
vijana wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) wakitambulishwa wakati wa semina ya
Ujasiriamali inayohusisha asilimia kubwa ya vijana jijini.
Pichani Juu na Chini ni
baadhi wa washiriki waliohudhuria wiki ya Ujasiriamali nchini. Mafunzo hayo
yameandaliwa na Shirika la Kazi Duniani ILO kwa kushirikirikana na Taasisi isiyo
ya Kiserikali ya ZAYEE.
Mgeni rasmi katika picha
ya pamoja na washiriki wa wiki ya Wajasiriamali nchini iliyozinduliwa rasmi jana
jijini Dar es Salaam itakayodumu kwa muda wa wiki nzima nchini.


Post a Comment