Shira la reli nchini
Kenya limezindua treni mpya ambayo ina mwendo wa kasi ili kutoa huduma kwa
wakazi wa viungani mwa mji wa Nairobi.
****************
Shirika
la reli nchini Kenya limezindua treni mpya ambayo ina mwendo wa kasi ili kutoa
huduma kwa wakaazi wa viungani mwa mji wa Nairobi.
Ni treni ya kwanza ya aina yake kuzinduliwa
tangu Kenya kujipatia uhuru mwaka 1963.
Treni hiyo itatoa usafiri kati ya mji mkuu na
mtaa wa Syokimau na viunga vyake, viungani mwa Nairobi ambako serikali imejenga
kituo cha treni ambacho ni cha kwanza kukamilishwa chini ya mradi wa ukarabati
wa mfumo wa reli ambao unafanyika kwa mara ya kwanza kwa miaka
80.
Treni hiyo inanuiwa kupunguza msongamano wa
magari mjini Nairobi ambao ni mojawapo ya miji unaokuwa kwa kasi barani Afrika
ukiwa na watu zaidi ya milioni tatu.
Rais Kibaki aliyefungua rasmi kituo hicho,
alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuipanda treni hiyo.
Kituo cha treni cha Syokimau ni cha kwanza cha
aina yake nchini Kenya, kikiwa na mashine za elektroniki zinazokagua vyeti vya
usafiri, pamoja na skirini kubwa ambazo zinatangaza safari za
treni.
Kila behewa lina uwezo wa kubeba abiria sabini
pamoja na miamoja na ishirini watakao simama.
Huduma hiyo itakuwa ya kasi na bora zaidi
ikilinganishwa na treni za hapo nyuma na pia zitatumia njia tofauti ya
reli.
Safari ya kutoka mtaa wa Syokimau inachukua
dakika kumi na tano kwa treni hizo huku ikiwa mtu atakwenda kwa gari itamchukua
hata masaa mawili. Itamgharimu abiria shilingi miambili kwenda na kutoka
mjini.

Post a Comment