Mzigo wa dawa za
kulevya.Picha na Maktaba.
Wafanyabiashara wawili wa
Jijini Dar es Salaam, wametiwa mbaroni Visiwani Zanzibar baada ya kupatikana
wakiingiza madawa ya kulevya kwa njia ya majini.
Naibu Mkurugenzi wa makosa
ya Jinai Zanzibar ACP Yusuf Ilembo, amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Othuman
Chande Othmani (22) mkazi wa Kinondoni na Abubakari Muharami Bakari(33) mkazi wa
Temeke.
Kamanda Ilembo amesema kuwa
watuhumiwa hao wote wamekamatwa katika Bandari ya Zanzibar walipokuwa wakiwasili
kwa boti kutoka Dar es Salaam wakiwa na madawa hayo ya kulevya aina ya
Heroine.
Amesema kuwa Mtuhumiwa
Abubakari alikamatwa juzi saa 3.00 asubuhi akiwa na kifurushi kimoja likichokuwa
na madawa hayo ambapo mwenzake Othman yeye ametiwa nguvuni leo saa 3.00 asubuhi
akiwa na vifurushi viwili vya madawa hayo aina ya Heroine.
Kamanda Ilembo amesema
kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na kuimarishwa kwa ulinzi na upekuzi wa
hali ya juu uliopo katika maeneo ya viwanja vya ndege na bandari ya
Zanzibar.
Amesema watuhumiwa hao
watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao za kupatikana na madawa ya kulevywa
visiwani hapa.
Amewataka wananchi wakiwemo
wasafiri wa ndege na boti wanaoingia na kutoka katika visiwa vya Unguja na Pemba
kuacha kulalama na kuona kuwa wanapopekuliwa
wanabughudhiwa.
Ammesema maeneo yote ya
Viwanja vya Ndege na Bandarini Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa
wengine wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimeimarisha ulinzi ili kuhakikisha kuwa
hakuna kitu cha hatari kinachoingizwa Visiwani humo.
Mbali ya Madawa ya kulevya
na silaha, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepiga mariufuku uingizwaji wa
mifuko ya plastiki ya aina zote na kwamba kwa yeyote atakayepatikana na mfuko wa
plastiki atakamatwa na kufikishwa mahakamani.
Kwa siku za hivi karibuni
baadhi ya wasafiri wamekuwa wakilalamikia hali ya upekuzi unaoendeshwa katika
maeneo ya Viwanja vya Ndege na Bandari na hali wanayoona kuwa ni usumbufu
kwao.
Post a Comment