WANANCHI
wa kata ya eneo la Kambarage kata ya Themi jijini Arusha wamemwandikia
barua kali mkuu wa wilaya ya Arusha,John Mongella huku wakilalamikia hatua ya
baadhi ya vigogo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha kuuza hovyo viwanja
mbalimbali vikiwemo vya wazi vilivyopo ndani ya eneo lao.
Wananchi hao wamevitaja
viwanja hivyo ni pamoja na kitalu nambari 10 ambacho kilitengwa kama eneo la
wazi sanjari na viitalu nambari 12 na 13 ambavyo vilitengwa kwa ajili ya makazi
yao.
Hatua hiyo inakuja zikiwa
ni siku chache tu baada ya baadhi ya watumishi wa jiji la Arusha kudaiwa kuuza
viwanja hivyo kwa kampuni mbili tofauti zinazomilikiwa na watanzania wenye asili
ya kiasia(majina yao yamehifadhiwa) zilizopo mkoani
Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa
zilizolifikia mtandao huu zimedai kwamba kufuatia hali ya sintofahamu wakazi hao
waliamua hivi karibuni kumwandikia barua mkuu huyo wa wilaya ya Arusha huku
wakimtaka aingilie kati sakata hilo.
Taarifa hizo zimedai
kwamba barua hiyo iliandikwa mnamo novemba 11 mwaka huu na kisha kufikishwa
moja kwa moja mbele ya ofisi ya kiongozi huyo huku ikilalamikia hatua ya baadhi
ya watumishi wa jiji la Arusha kutaka kupindisha haki ya umiliki wa viwanja
vyao.
Barua hiyo(Mwananchi ina
nakala yake) imesema ya kwamba wakazi hao wamekuwa wakiishi kwa muda mrefu kwa
hali ya wasiwasi huku ikienda mbali zaidi na kusema kuwa eneo la kitalu nambari
10 mbali na kuwa na chanzo cha maji limemilikishwa kwa mtu
binafsi.
“Kitalu nambari 10 yahusu
chemchem ya mto Themi ilitakiwa iachwe wazi na eneo la chemchem lihifadhiwe na
wananchi walioko vitalu nambari 12 na 13 walihifadhi kwa kupanda miti na
kuiboresha chemchem ikae katika hali ya usalama siyo imilikishwe kwa mtu
binafsi”ilisema sehemu ya barua hiyo
Hatahivyo,barua hiyo
ilienda mbali zaidi na kumtaka mkuu huyo wa wilaya kuupatia ufumbuzi wa haraka
mgogoro huo kwa kuwa una hatarisha usalama wa maisha yao kadri ya siku hadi
siku.
Mongella,alipofuatwa na
waandishi wa habari ofisini kwake alikiri wakazi hao kufikisha malalamiko yao
ofisini kwake hivi karibuni huku akisisitiza kwamba aliwapa maelekezo ya
kuwasilisha malalamiko yao kwa utaratibu unaotakiwa.
Hatahivyo,mkuu huyo wa
wilaya alisema kwamba amejiandaa kufanya ziara ya kutembelea maeneo yote yenye
mgogoro ili kushuhudia ukweli huku akihaidi kuyapatia ufumbuzi matatizo hayo
.
Post a Comment