Wanamgambo waliojihami kwa
bunduki, wamekalia bunge la Libya, kuelezea masikitiko yao kuhusiana na jinsi
serikali mpya ya nchi hiyo ilivyoundwa.
Wanamgambo hao wanataka
baadhi ya mawaziri kuondolewa, kwa sababu wanatuhumiwa kuwa na uhusiano na rais
wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.
Malori kadhaa, yakiwa
yamesheheni silaha za kutungulia ndege zimejipanga nje ya bunge la nchi
hiyo.
Libya iliandaa uchaguzi wa
amani mwezi Julai mwaka huu, na wanasiasa wa nchi hiyo waliafikiana kuhusu jinsi
ya kubuni serikali mpya siku ya Jumatano.
Waziri Mkuu Ali Zidan
alipataa uungwaji mkono kutoka kwa bunge la nchi hiyo kuhusiana na jinsi
alivyowachagua mawaziri wake.
Waziri huyo mkuu aliwateuwa
wanasiasa wasioegemea upande wowote na wenye misimamo ya kadri, katika baraza
lake ili serikali yake ya mseto ikubalike na pande zote.
Lakini mazungumzo hayo
yalivurugwa na maandamano mapema wiki hii na siku ya Jumatano, watu waliokuwa
wamejihami kwa bunduki, walivamia bunge la nchi hiyo na wamekuwa wakilidhibiti
tangu wakati huo.
Chanzo - BBC
Swahili
Post a Comment