Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano ,
Sayansi na Teknolojia Mh.January Makamba akitoa hotuba wakati wa hafla ya
utoaji tuzo kwa wanafunzi walioshinda shindano la kuandika Insha na Uchoraji
Sayansi (Dstv Eutelsat Star Awards) washindi wane kutoka shule za
sekondari walishinda baada ya kufanyika mchuano mkali ambao ulishirikisha
zaidi ya wanafunzi 1000 katika shule mbalimbali za Afrika nzima,shindano hilo la
tuzo liliandaliwa na MultiChoice kwa kushirikiana na Eutelsat
Communications.hafla hiyo ilifanyika kwenye Hotel ya Hyyat Kilimanjaro jijini
Dar es salaam.
Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya Multchoice ,Bi.Barbara Kambogi(kulia)katibu Mhutasi
Multichoice(kushoto)Revina Bandihai.wakifuatilia kwa umakini hotuba iliyokuwa
ikitolewa na Naibu waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia Mh.January
Makamba wakati akitoa hotuba katika hafla ya kuwapongeza washindi wa Dstv
Eutelsat Star Awards.
Majaji
wa shindano hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja katika hafla
hiyo.
Meneja
masoko wa Multchoice Furaha Samalu(kushoto)na Meneja masoko wa kampuni ya simu
Zantel Awaichi Mawalla.wakiwa katika hafla
hiyo.
Naibu
waziri wa Wizara ya Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia Mh.January Makamba
(watatu kushoto nyuma) Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter
Fauel(wakwanza kulia nyuma)wakiwa kwenye picha ya pamoja na vingozi
wengine,mbele kulia ni wanafunzi walioshinda tuzo ya Dstv Eutelsat
Star.
Meneja
Uhusiano wa kampuni ya Multchoice, Barbara Kambogi akiongea na waandishi wa
habari mara baada ya kumalizika kwa sherehe hiyo.PICHA NA
PHILEMON SOLOMON
Post a Comment