DARE
SALAAM, Tanzania
KATIBU wa Mkoa (CCM), wa Vyuo
vya Elimu ya Juu, Christopher Ngubiagai amewataka vijana wasomi wa mkoa huo wa
Kichama, kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano inayoendelea katika Mkoa wa Dar es
Salaam, ya kutoa maoni kwa ajili ya upatikanaji wa Katiba Mpya ya
Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo, Katibu huyo, amesema kuwa wasomi wana nafasi
nzuri katika kuchangia maoni yao bora ambayo yatasaidia kupatikana kwa Katiba
itakayolenga kulinda maslahi ya Watanzania kwa
ujumla.
Ngubiagai amesema maoni ya
wasomi yanahitajika katika mchakato huo wa upatikanaji wa Katiba Mpya si vyema
kwa vijana hao kujiweka pembeni huku wakitoa nafasi kwa watu wanye nia mbaya
kupandikiza maoni yao, kwa maslahi binafsi.
"Tunataka Katiba
itakayosimamia rasilimali, ardhi ya nchi hii, kulinda haki za makundi ya kijamii
hasa kila kijana pamoja na kudumisha amani na utulivu, udugu na
ujamaa,''alisema.
Ngubiagai alisema kila kijana
ana uwezo wa kupambanua mambo, hivyo ni vema wakatumia uwepo wa wajumbe wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba ndani ya Mkoa huo Dar es Salaam, kutoa maoni yao, vijana
hao wasomi wanapaswa kutumia muda huo vizuri.
Kutokana na hali hiyo, Katibu
huyo aliwataka viongozi wa matawi yaliyopo ndani ya taasisi ya vyuo vikuu nchini
kuhakikisha wanafahamu vizuri maudhui ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano iliyopo
sasa ili waweze kuwa na wigo mpana wa uchangiaji katika kutoa maoni
yao.
Post a Comment