![]() |
Yanga SC |
Na Mahmoud
Zubeiry
UHONDO wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unatarajiwa kuendelea leo, ‘Big Three’
zikijitupa uwanjani kuwania pointi za kutengeneza mazingira ya ubingwa mskmu
huu.
Mabingwa
watetezi, Simba SC watakuwa wageni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri
mjini Morogoro, wakati washindi wa pili wa ligi hiyo msimu uliopita, Azam FC
watakuwa wanaonyeshana kazi na washindi wa tatu, Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kweli hata
mchezo wa Morogoro utavuta hisia za wengi, lakini mchezo mkali zaidi na uliobeba
zaidi mustakabali wa msimamo wa Ligi Kuu utakuwa Dar es
Salaam.
Yanga na
Azam FC kwa sasa ni wapinzani wakubwa- na hapana shaka Watoto wa Jangwani sasa
wanaamini uzito wa mechi dhidi ya Wana Lamba Lamba ni sawa na uzito wa mechi
dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC.
Na bila
shaka ni kwa sababu hiyo, baada ya mechi yao na Mgambo JKT Yanga wakaenda kuweka
kambi katika hoteli ya Kiromo, Bagamoyo mkoani Pwani kujiandaa na mchezo wa leo.
Kwa kawaida,
Yanga huweka kambi Bagamoyo katikati ya Ligi, inapokuwa inajiandaa na mchezo
dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC hivyo kwa kwenda huko kuweka kujiandaa
na mchezo huo, maana yake wanaupa uzito sawa na pambano la
watani.
Wakati
vijana wa Yanga wakiwa Bagamoyo, Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mholanzi Ernie
Brandts Alhamisi alikwenda kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, kuifuatilia
timu hiyo ilipokuwa ikimenyana na Coastal Union ya
Tanga.
Katika
mchezo huo, Brandts aliyeambatana na Msaidizi wake, Freddy Felix Minziro alikuwa
makini kufuatilia uchezaji wa Azam na kunukuu kwenye kijitabu chake, maana yake
alikwenda kufanyia kazi katika mazoezi ya timu
yake.
Azam nayo,
ina ari mpya baada ya kurejea kwa kocha wake Muingereza, Stewart Hall aliyewapa
mafanikio makubwa uliopita.
Stewart
amerejea na ‘bonge la zali’ Azam, baada ya kuiongoza timu hiyo kuichapa Coastal
mabao 4-1 siku hiyo, ikitoka kuchapwa mabao 3-1 na Simba SC, chini ya kocha
aliyefukuzwa baada ya mechi hiyo, Mserbia, Boris
Bunjak.
Stewart
alifukuzwa Azam Agosti mwaka huu, baada ya kikiuka maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi
ya klabu, kwa kumpanga Mrisho Ngassa katika Fainali ya Klabu Bingwa Afrika
Mashariki, Kombe la Kagame dhidi ya Yanga. Yanga ilishinda 2-1 na kutwaa
Kombe.
Lakini
amerejeshwa kufuatia wachezaji wa Azam kuuandikia barua uongozi ya kumkataa
Bunjak na kupendekeza Muingereza huyo arejeshwe. Na uongozi wa Azam pia
ulizingatia kushuka kwa kiwango cha timu na kukubaliana na pendekezo la
wachezaji wake.
Azam
itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 4-1, uliowafanya wafikisha
pointi 21, baada ya kucheza mechi 10 na kurejea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa
Ligi Kuu, nyuma ya Simba na Yanga, zenye pointi 23 zote baada ya kucheza mechi
11, kila timu.
Yanga SC nao
watashusha timu yao wakiwa na kumbukumbu ya wimbi la ushindi katika Ligi Kuu
ikiwemo mechi ya iliyopita, ambayo waliichapa Mgambo JKT ya Handeni, Tanga mabao
3-0 Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuifikia kwa pointi Simba
SC iliyotoa sare ya 1-1 na Polisi mjini Morogoro siku
hiyo.
Faraja kwa
Yanga ni kurejea kwa wachezaji wake tegemeo, beki Kevin Yondan na mshambuliaji
Said Bahanuzi ‘Spider Man’, ambao walikuwa majeruhi. Yondan aliingia kipindi cha
pili katika mechi dhidi ya Mgambo, wakati Bahanuzi alipewa mapumziko zaidi,
ingawa leo anaweza kupangwa.
Kwa Azam
nako, faraja yao mbali na kurejea kwa Stewart, pia ni kurudi kwa mpachika mabao
wao tegemeo, John Bocco ‘Adebayor’ aliyekuwa anasumbuliwa na maumivu ya kifundo
cha mguu.
Wakati
Brandts akionyesha kutilia mkazo mechi hiyo kiasi cha kwenda hadi Chamazi
kushuhudia mbinu za wapinzani wake, Stewart naye alisema baada ya mechi ya
Coastal wanataka kuwafunga Yanga leo.
Katika
mchezo wa leo, bila shaka Stewart hatafanya mabadiliko makubwa kutoka kikosi
kilichotandika Coastal 4-1.
Langoni
anaweza kuendelea kusimama Mwadini Ally, kulia Samir Hajji, kushoto Ibrahim
Shikanda, katikati Aggrey Morris na Said Mourad katika safu ya ulinzi, Jabir
Aziz kiungo mkabaji, viungo wa pembeni Kipre Balou na Khamis Mcha ‘Vialli’,
kiungo mchezeshaji Salum Abubakar na washambuliaji John Bocco na Kipre Tcheche.
Brandts pia
hatarajiwi kuwa na mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake leo, kutoka kile
kilichoichapa 3-0 Mgambo JKT.
Utata tu
utakuwa baada ya kurejea Yondan, Mbuyu Twite atampanga pembeni au ataamua
kumuanzishia benchi mmoja kati ya mabeki wake watatu wa kati, mwingine akiwa ni
Nadir Haroub Cannavaro.
Leo bila
shaka Yawe Berko atadaka badala ya Ally Mustafa ‘Barthez’ na kama Twite
ataanzishwa kulia, maana yake Nahodha Nsajigwa Shadrack atapumzika, kushoto
Oscar Joshua, katikati wawili kati ya Twite, Cannavaro na Yondan, kiungo
mkabaji Athumani Iddi ‘Chuji’, viungo wa pembeni Simon Msuva na Hamisi Kiiza,
kiungo mchezeshaji Haruna Niyonzima na washambuliaji Said Bahanuzi na Didier
Kavumbangu.
Lakini
katika mechi za karibuni, Brandts amekuwa akitumia viungo wawili wakabaji na
mshambuliaji mmoja, ili kumfanya Niyonzima acheze zaidi na Frank Domayo ndiye
amekuwa akichukua nafasi ya mshambuliaji.
Haijulikani
katika mchezo wa leo kama Mholanzi huyo ataendelea na mbinu hiyo hiyo au ataamua
kutumbukiza washambuliaji wawili.
Mara ya
mwisho Yanga na Azam zilikutana katika fainali ya Kombe la Kagame, Agosti 10,
mwaka huu na Watoto wa Jangwani wakaibuka vinara na kutwaa Kombe kwa ushindi wa
2-1.
Mjini
Morogoro nako, nyasi za Uwanja wa Jamhuri zitahimilii vishindo vya Simba na
Mtibwa, ambao katika miaka ya karibuni, wamekuwa vibonde wa Wekundu hao wa
Msimbazi.
Simba
iliendelea kubaki mkoani Morogoro, baada ya sare ya 1-1 na Polisi Jumatano,
kujiandaa na mchezo wa leo, ikiwa imeweka kambi maeneo ya Nane Nane mkoani humo,
huku ikijifua kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro.
Wekundu hao
wa Msimbazi, wamepania kushinda mechi ya kwanza nje ya Dar es Salaam leo, baada
ya awali kutoa sare katika mechi zake zote za
ugenini.
Kwenye
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Simba ilitoka sare za bila kufungana na wenyeji
Coastal Union na Mgambo JKT kabla ya juzi kufungana 1-1 na Polisi, tena yenyewe
ndio ikihaha hadi kipindi cha pili kukomboa bao, baada ya Mokili Rambo
kutangulia kuwafungia Maafande hao kipindi cha
kwanza.
Mkombozi wa
Wekundu hao wa Msimbazi, alikuwa ni kiungo Amri Kiemba juzi, ambaye hilo
linakuwa bao lake la tano msimu huu.
Pamoja na
hayo, Simba inajivunia kuwa timu pekee ambayo hadi sasa haijapoteza mechi hata
moja katika Ligi Kuu, ikiwa inaongoza ligi hiyo kwa pointi zake 23 sawa na
Yanga, baada ya kucheza mechi 11, lakini ina wastani mzuri zaidi wa
mabao.
Zaidi ya
sare hizo tatu, Simba ilitoa sare nyingine mbili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,
dhidi ya Kagera Sugar ya Bukoba 2-2 na Yanga SC, wapinzani wao wa jadi,
1-1.
![]() |
Azam FC |
REKODI YA
YANGA AZAM FC:
Machi 10,
2012
Yanga 1 – 3
Azam
Septemba 18,
2011
Azam 1 – 0
Yanga
Machi 30,
2011
Yanga 2-1
Azam
Oktoba 24,
2010
Azam 0-0
Yanga
Machi 7,
2010
Yanga 2-1
Azam
Oktoba 17,
2009
Azam 1-1
Yanga
Aprili 8,
2009
Yanga 2-3
Azam FC
Oktoba 15,
2008
Azam FC 1-3
Yanga
![]() |
Simba SC |
REKODI YA
SIMBA NA MTIBWA TANGU 2005:
Machi 18,
2012
Simba 2 – 1
Mtibwa Sugar
Septemba 25,
2011
Simba 1 – 0
Mtibwa Sugar
Februari 27,
2011
Simba 4 – 1
Mtibwa Sugar
Feb 27,
2011
Simba 4-1
Mtibwa Sugar
Sept 29,
2010
Mtibwa Sugar
0-1 Simba
Machi 22,
2009
Mtibwa
Sugar 1-0 Simba
Sep 28,
2010
Simba
1-0 Mtibwa Sugar
Apr 21,
2010
Mtibwa
Sugar 0-4 Simba
Nov 15,
2009
Simba
3-1 Mtibwa Sugar
Feb 20,
2008
Simba
1-1 Mtibwa Sugar
Okt 7,
2007
Mtibwa
Sugar 1-3 Simba
2007:
Hazikukutana kwenye Ligi ndogo
Sept 10,
2006
Mtibwa
Sugar 1-1 Simba
Apr 9, 2006
Simba
1-1 Mtibwa Sugar
Okt 5,
2005
Simba
2-1 Mtibwa Sugar
Mei 22,
2005
Mtibwa
Sugar 0-1 Simba
![]() |
Mtibwa Sugar |
Post a Comment