Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizindua Ripoti ya Idadi ya
Watu Duniani kwa mwaka 2012, huko Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini
Unguja.
Idadi ya vifo vya akina
mama wajawazito imepungua kwa kiasi kikubwa hapa nchini katika miaka ya hivi
karibuni ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Hayo yamebainishwa na
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad wakati akizindua
Ripori ya Idadi ya Watu Duniani ya mwaka 2012 iliyofanyika Mkwajuni Mkoa wa
Kaskazini Unguja.
Katika hafla hiyo, Maalim
Seif alikuwa akimwakilisha Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohd
Shein.
Amesema ingawa vifo
vitokanavyo na uzazi duniani bado ni tishio, laikini kwa upande wa Tanzania
idahio hiyo imepungua kutoka vifo vya akina mama 578 katika mwaka 2004 na 2005
na kufikia vifo vya watu 473 mwaka 2006 hadi vifo 281 mwaka 2011, kwa kila mama
wajawazito 100,000.
Hata hivyo, Maalim Seif
amesema kuwa vifo hivyo viko juu katika mataifa mbalimbali
duniani.
Akizungumzia kwa upande wa
Zanzibar, Makam huyo wa Rais amesema vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi
usio salama vimepungua kutoka watu 473 kwa mwaka 2006 hadi kufikia vifo vya watu
281 kwa mwaka 2011, kwa kila akina mama 100,000.
kutokana na hali hiyo,
Maalim Seif amesema ipo haja ya jamii kuelimishwa zaidi juu ya umuhimu wa uzazi
salama na kupunguza vifo vya watoto na kuimarisha mpango kwa maendeleo ya taifa
letu.
Hata hivyo amesema jamii
bado haijatoa umuhimu unaostahili katika matumizi ya njia za uzazi wa mpango
salama hali inayopelekea kuwepo kwa ongezeko kubwa la
watu.
“Taarifa zinaonesha kwamba
Zanzibar hivi sasa inakadiriwa kuwa na idadi ya watu 1.3 milioni, wanaoongezeka
kwa kasi ya asilimia 3.1 kwa mwaka ambapo idadi ya watu katika kila kilomita
moja ya mraba imefikia watu 496 mwaka 2011”, ilieleza sehemu ya hotuba hiyo ya
Dkt. Shein iliyosomwa na Makamu wa Kwanza wa Rais.
Amesema kupungua kwa vifo
hapa nchini kunatokana na juhudi za serikali katika kuimarisha huduma za afya na
utoaji wa chanjo kwa akina mama na ikiwemo ya pepopunda na surua kwa mtoto
wachanga.
Kwa upande wao wawakilishi
wa Umoja wa Mataifa wameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuona
umuhimu wa huduma ya uzazi na kuamua kutoa huduma hiyo bila ya
malipo.
Mwakilishi Mkaazi wa
Shirika la Idadi ya watu (UNFPA) Tanzania bibi Mariam Khan amesema bado suala la
uzazi wa mpango linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na wanajamii
kuona ugumu juu ya matumizi ya njia za uzazi wa mpango.
Amefahamisha kuwa uzazi wa
mpango ni muhimu katika kusaidia kukuza kipato cha wanafamilia, sambamba na
kuwaendeleza watoto katika makuzi bora, na wito kwa jamii kutoa fursa
zinazostahiki kwa akina mama na watoto ili kusaidia harakati za maendeleo kwa
jamii.
Naye Waziri wa Afya wa
Zanzibar Mh. Juma Duni Haji, amesema wizara yake itaendelea na mpango wa utoaji
elimu kwa jamii ili kuongreza uelewa zaidi kwa wananchi wa Visiwa vya unguja na
Pemba.
Amesema akinamama na
watoto wanahitaji kulindwa kiafya, na kuwataka wazazi kushirikiana katika suala
la malezi na makuzi ya watoto.
Mapema akitoa muhtasari wa
ripoti hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Khamis
Mussa Omari, amesema zaidi ya wananwake milioni 222 duniani kote hawapati huduma
bora za mpango wa uzazi salama.
Amesema akina mama zaidi
ya milioni 80 hupata mimba zisizotarajiwa na kati ya hao akina mama 40 milioni
hutoa mimba na hata kuhatarisha maisha ya viumbe vilivyopo tumboni na mama
husika.
“Inakisiwa kuwa kiasi cha
mimba milioni 80 zinapatikana bila ya kutarajiwa duniani, huku nusu ya mimba
hizo zikitolewa, jambo ambalo ni hatari nyengine katika uzazi”. Alidokeza Katibu
Mkuu huyo.
Amesema uzazi wa mpango ni
miongoni kwa haki za binadamu lakini imeelekezwa zaidi kwenye haki za kifamilia,
ili wanafamilia waweze kupanga juu ya idadi na umri wa kupishana kwa watoto, ili
kuepuka mimba zisizotarajiwa.
Post a Comment