Kenya imejinyakulia kiti cha uwakilishi ndani Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa katika mchuano mkali kwa kupitia kundi la Afrika.
Pia Ivory Coast,Ethiopia,Gabon na Sierra Leone zinajiunga na baraza la haki za binadamu kwa ajili ya Afrika. Japani,Kazakhstan,Pakistan,Korea Kusini na Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ajili ya Asia. Brazil na Venezuela kwa ajili ya Amerika Kusini na Karibian Marekani na Ujerumani zimejishindia viti katika Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa katika mchuano mkali wa kundi la mataifa ya magharibi wakati Estonia na Montenegro zitajiunga kwa ajili ya Ulaya mashariki.
wanachama wa baraza hilo ambapo wanachama wanatakiwa wawe wenye kushikilia viwango vya juu kabisa vya kuheshimu haki za binaadamu. Na hivyo shirika la haki za binaadamu lenye makao yake mjini Washington Marekani la Freedom House limesema kwamba nchi saba zilizojipatia viti katika baraza hilo yaani Ivory Coast,Ethiopia,Gabon, Kazakhstan,Pakistan,Umoja wa Falme za Kiarabu na Venezuela hazistahiki kuwa wanachama. hata nchi nyengine tatu wanachama wapya wa baraza hilo za Brazil,Kenya na Sierra Leone sifa zake zinatajwa kuwa ni za kutiliwa mashaka