Kampuni ya MultiChoice imetangaza punguzo la
asilimia 10 ya malipo ya mwezi kwa wateja wa televisheni kwa vipindi vya DStv
litakaloanza kesho Novemba 15, 2012.
Meneja
Mkuu waMultiChoice Tanzania, Peter Fauel alisema punguzo hilo
litawawezesha wateja wao kulipia huduma za matangazo ya televisheni ya kituo
hicho kwa gaharama nafuu.
Fauel alisema kwa wateja
watakaokuwa wamelipia tayari huduma hiyo ndani ya mwezi huu, wataendelea kutumia
hadi pale mwezi utakapokuwa umeisha, kisha wataanza na bei mpya ya punguzo
kuanzia mwezi unaofuata ila wahakikishe huduma yao
kutokatika.
“Tumedhamiria kuwapunguzia
wateja wetu gharama kubwa kulingana na hali halisi ya maisha ya mwananchi wa
kawaida,” alisema Fauel.
Meneja mkuu huyo alisema,
kuwa kama kawaida yao huwapa wateja wao unafuu wa bei kulingana na kipato chao,
hivyo punguzo hilo litawanufaisha kwa kiwango kikubwa ili kila mmoja afaidi
burudani.
Alisisitiza kuwa DStv
itaendelea kuwapatia Watanzania na Waafrika kwa ujumla vipindi vyenye ubora kwa
vile wamewekeza katika vipindi vipya.
Kwa wateja watakaonufaika
na ofa hii, wataweza kupunguza gharama za kulipia huduma yao ya DStv kwa 150,000
kwa mwaka!
Fauel akaongeza kwamba
“Tunawaahidi wateja wetu huduma bo ra na kwamba kwetu mteja ni mfalme. Mtandao wetu wa
usambazaji unazidi kupanuka na sasa tupo kila mkoa wa nchi. Pia tunafurahi
kwamba sasa tuna ofisi zetu Kariakoo na supermarket ya Uchumi iliyopo barabara
ya Pugu. Hii itawarahisishia wateja wetu kupata bidhaa na huduma zetu kwa haraka
zaidi.
Post a Comment