Akizungumza na paparazi wetu jijini Dar juzi, Aisha alisema ingawa bado anaendelea kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kumeza dawa lakini amepata kazi ya uhamasishaji katika Shirika la Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Ukimwi (PHRP) lililopo Kinondoni
Aidha, alisema kazi hiyo ya uhamasishaji anaifanya kwa wiki mara tatu ambapo ni Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Alisema hutoa somo kwa waathirika wa unga wanaoishi katika kituo hicho.
Aisha aliongeza kuwa, somo analotoa linahusu umuhimu wa kuzingatia dawa na jinsi ya kusahau utumiaji wa unga kwa vile imebainika kuna wakati waathirika walioamua kuacha, hutamani kuendelea kutumia.
“Namshukuru Mungu sasa hivi kipimo cha dawa kimepungua kwa sababu nilipoanza nilikuwa nakunywa kikombe kizima, kwa sasa nakunywa nusu kutokana na afya yangu kuendelea vizuri, lakini pia nimekuwa muhamasishaji wa PHRP kwa kutoa somo kwa waathirika,” alisema.
Alimpongeza mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ kwa uamuzi wake wa kukubali kuanza kutumia dozi ambapo sasa afya yake imerudi vizuri tofauti na siku za nyuma.
chanzo:globalpublisher
Post a Comment