Na Mroki Mroki, Arusha
MAPOKEZI ya Kihistoria katika jiji la Arusha yamefanyika leo
wakati wafuasi, Mbunge wa Arusha Mjini kwa Tiketi ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema walipo miminika kwa Wingi
kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) hadi katika Viwanja
vya Kilombero mjini hapa alipohutumia maelfu ya wana CHADEMA Arusha Mjini.
Mapokezi yahoo yamefanyika wakati Godbless Lema alipokuwa
akirejea mjini Arusha akitokea jijini Dar es Salaam kusikiliza hukumu ya Rufani
ya Keshi yake ya Kuvuliwa Ubunge iliyotolewa maamuzi ya kumrtejeshea Ubunge
wake Desemba 21,2012.
Maelfu ya wananchi wakiwa katika msafara mrefu zaidi ya
pikipiki 500 na magari ulianzia Uwanja wa Ndege KIA mara baada ya Mbunge huyo
kuwasili uwanjanai hapo majira ya saa 4:20 Asubuhi.
Wafuasi wa Lema wakishangilia barabarani wakati Mbunge huyo akipita.
Mbwembwe za waendesha pikipiki wengine ziliwashinda na kuanza kuanguaka.
Furaha hiyo ilikuwa kwa kilu aliye Mwanachadema
Skafu na vitru mbalimbali vilivyo na alama ya CHadema viliuzwa jijini Arusha kwa wingi.
Mke wa Mbunge Godbless Lema akiwa kwenye gari pamoja na mtoto wao wakati wa mapokezi hayo.
Lema Arusha anafananishwa na Barack Obama
Watu walining'inia katika magari bila hofu
Lena akiwa nba Mbunge wa Arumeru Mashuari CHADEMA, Joshua Nasari.
Wafuasi
wa chadema wakiwa eneo la ofisi za manispaa wakati wa shamrashamra za
kumpokea mbunge wao aliyeshinda rufaa yake jana jijini dar es salam..
msafara wa lema ukikaribia arusha mjini
2 comments
ALIVYOSEMA TUNDU LISU KUWA MAJAJI HAWANA UWEZO NI KWELI KUMBE NDIO SABABU JAJI MKUU ALIJITOA KUSHIRIKI KESI HII MAHAKAMA YA RUFAA
ReplyUSAWA WA KIJINSIA TANZANIA ZIIIIIIII
ReplyPost a Comment